Mshambuliaji wa Barcelona, Leo Messi amesema ameshangazwa na watu wanaosema amechangia kwa kocha mpya Gerardo Martino kujiunga na timu hiyo.
"Sijui lolote kuhusu kocha, nimesikia wakisema nilishawishi aje, lakini hilo lilikuwa ni suala juu ya uwezo wangu na uongozi ndiyo ulikuwa na uamuzi kwa kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
"Naweza kusema simjui kocha na sijawahi kukutana naye hata mara moja. Ninachojua amekuwa kocha mwenye mafanikio akiwa na Newell Old Boys na timu ya taifa ya Paraguay. Kwangu ni jambo zuri,” alisema Leo.
Kabla ya kocha huyo maarufu Tata, kujiunga na Barcelona kulikuwa na taarifa kuwa Messi alikuwa akimpigia debe ajiunge na timu hiyo kwa kuwa ni raia wa Argentina lakini pia alikuwa anafundisha timu iliyomlea ya Newell Old Boys.
Lakini Messi aliondoka Argentina akiwa na miaka 13 kabla ya kocha huyo hajaanza kuifundisha na akapelekwa Hispania kwa matibabu na baadaye kujiunga na Barcelona.
0 COMMENTS:
Post a Comment