July 27, 2013

MWADINI AKITIBIWA BAADA YA KUUMIA
Kipa Mwadini Ali wa Azam FC ameumia leo katika mazoezi ya mwisho ya Stars yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mandela jijini Kampala, Uganda.

Mwadini aliumia enka baada ya kugongana na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Kutokana na kuumia huko, Mwadini alitibiwa kwa takribani dakika 15 na daktari Mwanandi Mwankemwa.

Baada ya hapo alifungwa bandeji ngumu na kutoendelea na mazoezi, hali iliyoonyesha alikuwa anatakiwa kupumzika.


Majeruhi mwingine ni Mcha Hamis ‘Vialli’ aliyeumia goti katika mazoezi kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza lakini leo angalau alipiga hata danadana.
MCHA MAZOEZINI UGANDA...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic