Matumaini
ya Watanzania kwa Taifa Stars huenda ingeweza kubadili matokeo mjini Kampala na
kusema mbele kucheza Kombe la Chan mwakani nchini Afrika Kusini, yameishia
hewani.
Stars
imelalala kwa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wake The Cranes mjini Kampala na
kufanya iwe imepoteza kwa jumla ya mabao 4-1.
Stars ambayo
ilipoteza mechi ya kwanza kwa bao 1-0 jijini Dar, leo ilikwenda mapumziko ikiwa
na inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Amri Kiemba.
Lakini kipindi
cha pili Waganda walionekana kubadilika na mapema tu wakapata bao la kwanza na
bao la pili lililofungwa kwa mkwaju wa penalti.
Kosa la
kuzubaa na mpira wakati Stars inashambulia kuliifanya Uganda ifanye shambulizi
la kushtukiza na kufunga kwa ulaini bao la tatu.
Baada ya
hapo, wenyeji walionekana kupoteza muda huku wachezaji wa Stars wakimlalamikia
mwamuzi kutokana na kuonyesha wazi alitaka wenyeji washinde.
Mara ya mwisho The Cranes kupoteza mechi katika Uwanja wa Namboole ilikuwa ni mwaka 2004 walipofungwa na Afrika Kusini na baada ya hapo wamekuwa wakishinda au kutoka sare.
Hata hivyo,
Stars pia ilionekana kukosa mipango kila ilipofika mbele kama ilivyokuwa katika
mechi ya kwanza jijini Dar.
Wachezaji
wa Stars waliendelea kucheza kama wale waliokata tamaa kabisa na mara nyingi
walipokonywa mipira karibu kila mara.
Baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, Kocha Mkuu, Sredojevic Milutin 'Micho' aliyewahi kuinoa Yanga alionekana kuchanganyikiwa kwa furaha na kukimbia kama mwendawazimu.
Mara ya
mwisho Stars ilicheza michuano ya Chan mwaka 2009 nchini Ivory Coast na
ikatolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na
Zambia mjini Bouake.
Poor Tanzania. Bravo Uganda.
ReplyDelete