Kiungo nyota wa Real
Madrid, Xabi Alonso amerejea mazoezini kwa mara nyingine ikiwa ni zaidi ya
mwezi mzima kuwa nje ya uwanja.
Alonso alikuwa nje
ya uwanja kutokana na kufanyiwa upasuaji na sasa ni kati ya wachezaji walio
katika mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya PSG,
leo.
Madrid wameonekana
kuwa na faraja kubwa baada ya kiungo huyo aliyezaliwa katika eneo la Tolosa
kurejea tena mazoezini.
Kwa upande
mwingine, taarifa kutoka katika uongozi wa Real Madrid zimeeleza kuwa kiungo
Mbrazil, Kaka amekuwa akiendelea vizuri zaidi na kuwapa matumaini kuwa atarejea
katika kiwango chake.
0 COMMENTS:
Post a Comment