Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ leo amemuonyesha Emmanuel Okwi fulana yenye maandishi
yanayomnanga.
Kaburu aliyekuwa makamu mwenyekiti wa
Simba kabla ya kujiuzulu miezi kadhaa iliyopita, alimuonyesha Okwi jezi hiyo
aliyokuwa amevaa.
Jezi hiyo ilikuwa imeandikwa, “I always
remember Mafisango, who is Okwi?” (Kila mara namkumbuka Mafisango, kwani Okwi ndiyo nani?).
Okwi alipokwenda kuwasalimia upande wa benchi la Simba, Kaburu alimuonyesha Okwi
maandishi hayo, akaonyesha kushtuka lakini baadaye wakakumbatiana.
Okwi alikuwa katika kikosi kilichoifunga
Yanga mabao 5-0 pamoja na Mutesa Mafisango ambaye alifariki dunia wiki chache
baadaye kwa ajali ya gari jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment