January 13, 2014

RAGE

Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Daniel Kamna amesema mwenyekiti wao aliyerudishwa madarakani na TFF, Ismail Aden Rage ndiye aliyesababisha wafungwe katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi.


Simba imefungwa bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi na KCC ya Uganda ambayo imelipeleka kombe hilo jijini Kampala.
Akizungumza kuhusiana na hilo, Kamna alisema Rage hakuwahi kwenda kuiunga mkono timu hata mchezo mmoja.
KAMNA

“Kitendo chake cha kuja kwenye fainali ndiyo kimeleta matatizo makubwa, vijana wamemuona wakawa kama wameishiwa nguvu.
“Wanajua namna watu wa kamati ya utendaji wanasumbuka na timu, kumuona Rage wakaona kama hali imebadilika.
“Haikuwa hali ya kawaida, siku zote anasubiri timu ifikie mafanikio basi ajitokeze kwa ajili ya kujisifia,” alisema Kamna akionekana kuwa na jazba.
Baadhi ya mashabiki wa Simba walizichapa baada ya mechi ya fainali, baadhi wakiwashutumu wenzao kuwa wafuasi wa Rage na walitaka kuwaangusha kwa makusudi.

Simba ilifika fainali ya michuano hiyo bila ya kufungwa hata bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic