September 17, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa wachezaji wawili Mganda, Juuko Murushid na Mrundi, Haruna Niyonzima wataanza mazoezi wiki hii.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, ameeleza wachezaji hao wataungana na wenzao waliokuwa kwenye mchezo wa ligi Mtwara dhidi ya Ndanda FC.

Manara amesema Niyonzima na Murushid wataanza rasmi kujinoa na kikosi cha Simba tayari kuanza maandalizi ya kucheza mechi zijazo za ligi na mashindano mengine.

Niyonzima na Murushid hawakuwa na timu ya Simba kutokana na sintofahamu baina yao na uongozi wa klabu iliyopelekea kukosekana kwenye timu.

Tayari wachezaji hao walishakutana na mabosi wa Simba kupitia kwa Kaimu Rais, Salim Abdallah 'Try Again' na kuweka mambo sawa ambapo sasa wataanza kujifua wiki hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic