February 25, 2021

 


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola mabao yake matatu yamempoteza mshikaji wake Luis Miquissone wa Simba mwenye mabao mawili katika kucheka na nyavu ndani ya uwanja licha ya kutumia dakika kiduchu.

Luis amecheza jumla ya mechi 14, mechi 9 ameyeyusha dakika 90 zote na kumfanya atumie dakika 810 huku mechi tano akitumia jumla ya dakika 383. Jumla ametumia dakika 1,193 akikosekana kwenye mechi nne.

 Mabao yake mawili kati ya 42 ambayo yamefungwa na Simba, aliwafunga JKT Tanzania na kushangilia kwake kulisababishwa aonyeshwe kadi ya njano.Bao la pili aliwafunga Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Wakati Luis akifanya yake, Carlinhos amefunga matatu kwenye mechi sita ambazo amecheza kati ya mabao 34 yaliyofungwa na timu yake. Ametumia jumla dakika 346 na ni mechi mbili pekee alianza kikosi cha kwanza huku nyingine nne akitokea benchi.

 Bao lake la kwanza aliwafunga Coastal Union, bao la pili aliwafunga Namungo FC na bao la tatu aliwafunga Mtibwa Sugar.


 Pia mbali na kumpoteza kwa upande wa kucheka na nyavu ameweza kuwa na nidhamu kwa kuwa hana kadi hata moja ya njano tofauti na Luis ambaye ana kadi mbili za njano ile ya kwanza alionyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

 Za Luis hizi hapa:-Mtibwa Sugar dk 90
Biashara United dk 90, Gwambina dk 90.
JKT Tanzania 79, Dodoma Jiji, 79, Prisons 90. Ruvu Shooting dk 90.
 Mwadui dk 90
Kagera Sugar dakika 90Yanga dk 90, Polisi Tanzania dk 90Ihefu 79Dodoma Jiji 60 na Azam FC 86.

Carlinhos ndani ya ligi:-Mbeya City dk 30Kagera Sugar dk 35, Mtibwa Sugar dk 72Coastal Union dk 90 , Namungo FC dk 90Mtibwa Sugar 29.

17 COMMENTS:

  1. Unafananisha watu tofauti.hata robo hafiki hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtasubili saaana huwez kumlinganisha luis miquson na ujinga huo hata kdogo

      Delete
  2. umeanza tena upuuzi wako mahaba na timu yako ya mchangani inaonekana ushindi wa Simba kimataifa unakuuma sana. Uliwalinganisha Lamini Moro na Wawa wakati simba imefungwa magoli mengi kuliko yanga ila sasa yanga imefungwa magoli mengi kuliko Simba hujarudia kuwalinganisha.
    Hiyo timu yako kiwango kitabaki hivyohivyo na si muda mrefu tunawaondoa kileleni.

    ReplyDelete
  3. hahahahahahah endelea kuwafarijii...

    ReplyDelete
  4. We uliyeweka hizo unakosa adabu kabisa kumfananisha mikson na karinho unatakiwa intake radhi mikson afu mambo yakuwa mnawafananisha mchezaji champion league na mchezaji wa bwawan ni kukosa weredi wa kaz ysko

    ReplyDelete
  5. Takwimu (data) jamani... msijipofushe hapo!

    ReplyDelete
  6. Inaonekana we mwandishi hukuenda shule, inabidi tukupeleke drsn. Unaushabiki kuliko weredi wa kazi yako.kumbuka hiyo ni kazi unajiharibia cv yako.

    ReplyDelete
  7. Jinga moja lisilojitambua nenda kaombe pale utopoloni nafasi ya usemaji inaweza kukufariji pumbavuuu

    ReplyDelete
  8. Mwacheni ajifariji. Utopolo roho za kwanini zinawauma sana.Simba anafanikiwa ,Namungo anafanikiwa.Wao tia maji maji wazee wa kususa.

    ReplyDelete
  9. Mwandshi cjui km unaakili tmamu kwa kumfananisha mikison na maembe

    ReplyDelete
  10. Jamani 27.2B anafananishwa kweli not serious

    ReplyDelete
  11. Nmecheka kifara eti amepoteza Luis labda Luis wa buza

    ReplyDelete
  12. Mbona humfananishi na sapong alocheza game zote

    ReplyDelete
  13. Huyu jamaa kamaserikali ikijua anaweza hukumiwa kwa kumfananisha Miquison na vitu vya kisenge kisenge

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic