February 27, 2021


RAHEEM Kangezi,'Zamuda' Mwenyekiti wa Klabu ya African Lyon na mmiliki wa timu hiyo amesema kuwa wamefanya mambo mengi kwa ajili ya Simba ikiwa ni pamoja na logo mpya ya timu hiyo pamoja na mpango wa Visit Tanzania.

Zamuda amesema kuwa ikiwa wanasema kwamba anapiga porojo hilo sio kweli kwa kuwa anamheshimu kila mtu ikiwa ni pamoja Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Jana timu yake ilipoteza kwa kufungwa 0-3 dhidi ya Simba huku akiweka wazi kwamba kuna vitu aliahidiwa kulipwa na bosi wa timu yao ila havijafanyika mpaka sasa. 

"Tunafanya vitu vingi sana ndani ya Simba kwa kuwa ile Visit Tanzania imetoka kwetu na muulize Barbra (Gonzalez) akuonyeshe email ambayo nilimtumia pia logo mpya ya Simba imetoka kwetu.

"Tuna wachezaji ndani ya ligi zaidi ya 50, Miraji Athuman ametoka kwetu, kuna Mwenyekiti wa Mashindano wa Yanga ametoka kwetu na kocha msaidizi pia ametoka kwetu.

"Bajeti yetu sio kubwa lakini ni tofauti kidogo kwa kuwa ninawalipa wachezaji na ninasafirisha wachezaji na kusomesha pia," amesema.

11 COMMENTS:

  1. Sasa siangeweka kwenye timu yake pumba tupu

    ReplyDelete
  2. Haya tumekusikia peleka malalamiko yako CAS

    ReplyDelete
  3. Kumbe ni wazuri kwa Kudesa.. hehehe.

    ReplyDelete
  4. Kuiga iga tu then mnajita next level makuma fc nyie

    ReplyDelete
  5. Huyo Raheem ni tapeli tu .Anajulikana ni Utopolo na alipewa pesa ya kambi na GSM na akaahidi ushindi.Povu lote ni kashindwa kutimiza ahadi.Jamaa wanataka pesa zao.

    ReplyDelete
  6. Kama Logo, Simba walitangaza kwa yeyote anayeweza kubuni logo mpya anakaribishwa. Kwa hiyo sio wewe tu uliyepeleka logo simba ila tu yako imekubaliwa

    ReplyDelete
  7. Raheem ana wivu na mafanikio ya Simba SC,baada ya mechi kwisha ameongea pumba nyingi sana. Nafikiri matokeo yamemchanganya ni kumsamehe tu.

    ReplyDelete
  8. Sasa kwan kutoa idea ya logo ni dhambi? Au mlitaka akaekimya muwape sifa watu wengine kumbe wameletewa tu wao Kazi yao kutangaza, na yeye amesema baada ya kauli ya dhihaka juu yake

    ReplyDelete
  9. Suala la logo ilitolewa tenda kabisa, watu kibao walituma design zao labda na yeye yumo. Ila visit Tanzania mbona hilo neno liko tuu kila mahali, visit rwanda, visit malaysia n.k.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic