OFISA Habari wa Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Bara amewaomba Watanzania wamuombee kwa kuwa kwa sasa hali yake haijatengamaa kwa kile ambacho ameambiwa na madaktari kuwa amekula chakula chenye sumu.
Kupitia ukurasa wake wa Istagram Masau Bwire ameandika:Kwa siku kadhaa zilizopita, nimekuwa sipokei simu, au nikipokea nasema tu siko vizuri, siwezi kuzungumza! Wapo walionielewa, lakini wapo walioona kama ni jeuri na kiburi tu, nafanya makusudi, kwa sababu sitaki kuzungumza nao.
Niwaombe radhi, wanisamehe kwa yote, lakini pia niwaaambie, na kuwahakikishia kwamba, sina kawaida hiyo ya kutopokea simu ya mtu yeyote atakayenipigia, siwezi kudharau simu ya mtu yeyote, daima namuomba Mungu, aniepushe na tabia hiyo ya kishetani ya kudharau na kutowapa ushirikiano pale wanapohitaji lolote kutoka kwangu.
Kwa kweli nilikuwa katika hali ngumu, kama unavyoiona hiyo picha, ndio uhalisia wa namna nilivyokuwa, nilikamatika haswa! Baada ya vipimo vya Hospitali, wataalamu wa afya (Daktari), walinambia, nilikula chakula ambacho hakikuwa salama, chenye sumu!
Mwili pamoja na kwamba, haujawa na nguvu ya kutosha, hata kazini bado sijaweza kwenda, namshukuru Mungu, kwa kweli sijambo, naendelea vizuri.
Nikumbukeni katika maombi.
Pole sana na Mwenyezi Mungu akuponye
ReplyDeletePole sana kiongozi Mungu akupe wepesi upone haraka
ReplyDeletePole sana,,,Mungu akuponye
ReplyDeleteMungu akuponye
ReplyDeletePole mwanampira mwenzetu. Mungu akuponye
ReplyDeletePole Sana Msemaji.
ReplyDeleteMungu atakuponya tena kutoka kindani
Kiki tu hiyo Mgonjwa ana simu kwenye paja??
ReplyDeletePole sana, ila punguza kula mihogo pori
ReplyDeleteHILI JAMAA NI PUMBAVU SANA WATU HAWAJAGUNDUA TU
ReplyDeleteKwa nini
ReplyDeleteNakubaliana na wewe Anapenda kiki tu Angalia hiyo picha kwa makini.Ipi staged.Ni ya kupanga.Simu kwenye paja.Alivyolala.
ReplyDeleteSasa nyie mikia fc imekuwaje tena kutaka kumtoa roho mzee wa kupapasa>?
ReplyDeleteWewe mbwa una ushahidi wa hayo unayosema?Utopolo ukiitwa kutoa ushahidi utaweza kuutoa.TCRA kutoa IP ya simu au Internet iliyotumika kuandika huu uzushi utajibu nini?
ReplyDeleteUtopolo wakati mwingine kaa kimya.
Sasa huyu naye kuna mtu anashida nae hadi ahangaike kumtoa roho? Uroho wake ndip umemfanya afakamie vyakula vyenye viwango cha chini ndio yakampata hayo kama ni kweli anyway
ReplyDeleteNi kiki tu hamna lolote.Mtu wa kawaida hatembei na simu 6.
ReplyDelete