Na Boniface Wambura
Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia
(Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika (Afcon) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.
Stars na
Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA).
Makubaliano
ya kucheza mechi hiyo yamefikiwa kutokana na mazungumzo kati ya Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Chama cha
Mpira wa Miguu Namibia (NFA), John Muinjo.
Benchi la
Ufundi la Brave Warriors linaongozwa na kocha mzawa Ricardo Mannetti, na mechi
hiyo itachezwa ama Uwanja wa Sam Nujoma au Uwanja wa Uhuru jijini Windhoek.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inafundishwa na kocha Kim
Poulsen kutoka Denmark na inatarajia kuanza kucheza mechi za mchujo za AFCON
Septemba mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment