Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm
ametua salama nchini Uturuki.
Akizungumza kutoka Antalya, Uturuki, Msemaji
wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema tayari kuna alikuwa amekwenda kumpokea kocha
huyo uwanja wa ndege.
“Tunaamini atakuwa amewasili, alitarajia
kufika hapa saa tisa na nusu ya Afrika Mashariki.
“Sisi tuko mjini na kuna mtu amekwenda
uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea,” alisema Kizuguto.
Van Der Pluijm amekwenda Uturuki kupitia
Rwanda baada ya kukosa ndege jijini Dar.
Kesho ataishuhudia Yanga kwa mara ya kwanza ikicheza mechi
ya kirafiki dhidi ya Altay FK ikiwa ni ya pili baada ya kuanza ya kwanza na
ushindi wa mabao 3-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment