Kocha Zdravko Logarusic amefurahia
kusikia mmoja wa wagombea wa urais Evans Aveva akisema wataendelea kufanya naye
kazi.
“Nimepata ofa mara mbili lakini bado
niliendelea kusubiri Simba wamalize uchaguzi. Sasa nimesikia hata wagombea wa
urais wamesema wanatafanya kazi na mimi.
“Nimesoma kwenye mitandao, jambo
zuri kwangu na inanipa moyo wa kufanya kazi kwa juhudi zaidi nitakaporejea.
“Unajua mtu akionyesha kukuamini ni
deni kubwa kwao, hii ndiyo ipo kwangu. Lakini sina hofu na Simba msimu ujao
kuwa itafanya vizuri,” alisema Logarusic.
Logarusic ndiye alikuwa kocha wa
Simba kwa nusu msimu akichukua nafasi ya Abdallah Kibadeni aliyeanza nayo
msimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment