Kitendo cha Yanga jana kucheza mchezo wake wa 15 wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Simba ikiwa na mechi 12, kimezua maswali mengi huku lawama za Yanga zikienda kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPLB).
Hivi sasa Simba ina michezo mitatu nyuma ya Yanga kutokana na kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Desemba 15 mwaka huu itacheza ugenini dhidi ya Nkana FC ya Zambia kabla ya kurudiana Desemba 21 Dar es Salaam.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amehoji kisa cha wapinzani wao kutocheza mechi ndani ya wiki mbili baada ya wao kurudi kufuatia kucheza mechi yao ya kimataifa.
"Yanga wakati tunacheza kombe la Shirikisho tuliporudi Kenya tulicheza baada ya siku mbili Shinyanga na baada ya hapo tukaenda Mbeya baada ya siku tatu tukaenda Rwanda," alisema.
Ofisa habari wa TFF, cLIFORD Ndimbo alisema kuwa mipango ya Ligi kuu itakwenda sawa kwa kuwa kila kitun nni mpangilio.
Hivi sasa Simba ina michezo mitatu nyuma ya Yanga kutokana na kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Desemba 15 mwaka huu itacheza ugenini dhidi ya Nkana FC ya Zambia kabla ya kurudiana Desemba 21 Dar es Salaam.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amehoji kisa cha wapinzani wao kutocheza mechi ndani ya wiki mbili baada ya wao kurudi kufuatia kucheza mechi yao ya kimataifa.
"Yanga wakati tunacheza kombe la Shirikisho tuliporudi Kenya tulicheza baada ya siku mbili Shinyanga na baada ya hapo tukaenda Mbeya baada ya siku tatu tukaenda Rwanda," alisema.
Ofisa habari wa TFF, cLIFORD Ndimbo alisema kuwa mipango ya Ligi kuu itakwenda sawa kwa kuwa kila kitun nni mpangilio.
Yanga hawana haja ya kulalamika au kuingia mchecheto kwani kiuhalisia Simba ndio wa kulalamika kutokana na hali ilivyo kwa sababu kwa bodi yetu hii ya ligi kuna uwezekano mkubwa SIMBA kuja kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja. Wanaosema mbona Barcelona anacheza ligi na mashindano ya kimataifa pia, ni watu kama wanaota vile kuyalinganisha mazingira ya Spain au Barcelona na Tanzania. Kwanza kutokana na timu zetu kutofanya vizuri katika mashindano ya Africa kwa miaka mingi Taifa au nchi kupitia taasisi husika ina kila sababu kuvijengea mazingira rafiki vilabu vyetu vinavyoshiriki mashindano ya Africa kuhakikisha vinafanya vizuri kwani povu lote la wadau wanalotoa kuhusiana na ratiba ya ligi lengo lake ni kumpata mshiriki wa mashindano ambayo Simba na mtibwa wanaashirki. Ingekuwa vizuri malalamiko hayo yangelalamikiwa kabla ligi kuanza ili kuweka mazingira ya ratiba ya ligi bila kuathiri ushiriki wenye tija kwa vilabu vyetu kimataifa. Kwa mfano wapinzani wa Simba Nkana FC hawashiriki mashindano yoyote hivi sasa kwakuwa ligi ya Zambia haiajaanza. Utaona jinsi gani walivyo na mazingira rafiki ya ushiriki mechi zao za awali za kimataifa. Hatua hizi za awali za mashindano ya Africa kiuhalisia ni ngumu mno kuliko hatua za makundi na ndipo mara nyingi vilabu vyetu vinapofeli kwa hivyo si busara kuanza kuwachanganya washiriiki wetu kisaikolojia labda kama kuna watu wangefurahia kuona timu zetu zinatolewa mapema katika mashindano ya vilabu vya Africa na hapana shaka yoyote kutokana na nature ya akili zetu za kutawaliwa za kitanzania wapo watu wanaotamani Simba isiende popote siwezi kuuita ushabiki wa kipinzani isipokuwa ni roho chafu za husda. Kufanya vizuri kwa timu zetu kimataifa ni agizo la muheshimiwa Raisi ni ajenda ya Taifa kuhakikisha Tanzania na watanzania wanaachana na Ulaza na kuwa watu wa ushindani na kamwe hatuwezi kuwa watu wa ushindani kimataifa kama tutashindwa kuungana mkono na kuwa kitu kimoja ili kujengeana mazingira ya ushindi lakini kama kila mtu atauweka ubinafsi wake mbele na kuacha kukubali yakwamba mtanzania akifanya vizuri na yeye ni mtanzania pia basi Taifa hili na wananchi wake wataendelea kuteseka.
ReplyDeleteHuu ni ujinga uliokithiri kwa klabu kubwa kama yanga kulalama,tena ni upumbavu wa kiwango cha juu kabisa mnataka kusema tayari mlishasahau juzi tu hapa kabla hamjatolewa mlikua na viporo vitatu je mlimsikia simba akilalama?acheni ujinga yanga soka haliko hivyo au kunya anye kuku akinya bata kaharisha.
ReplyDeleteTumia kichwa kuongea sio pua kwa makamasi,umesahau miaka 3 yote ya huko nyuma Mikia FC ilikuwa ikilalama kuhusu viporo vya Mabingwa wa kihistoria?
DeleteHiyo ndio tabia za mpira waTz ambazo hazitupeleki mbele Zaidi ya ushirikina kama wafanyao ndugu zako Simba,wachawi wakubwa!
Suala la kimataifa ni la wote sasa kama unaomba dua ili simba watolewe sawa ni uzalendo pia.
ReplyDeleteHoja za Yanga ni za msingi sana iweje wao hawakupewa muda hata wa kupumzika na walikuwa na ratiba ngumu sana wakati Simba wao wanapewa kwa kuondoa ushabiki usio na maana sio vyema kukashifiana ila ni vyema pakajengwa hoja za msingi,na sharia iliyotumika kuweka presha kwa Yanga mwaka jana leo iko wapi?
ReplyDeleteSio za msingi...kinachotokea sasa ndio kilikuwa kwa Yanga mwaka Jana..Kama ingekuwa Simba imecheza mechi nane mfululizo Dar...Zahera angelalamika sana
Deletekwakua wewe umetendewa vibaya unaombaa na jirani yako atendewe hivyo hivyo roho mbaya hiyo maana ukitolewa jicho moja unaomba na rafiki yako atolewe yote mawili?
DeleteHawakupewa muda wakupumzika kivip?acha kubwabwaja ndugu,yanga mpaka wanatolewa walikua na viporo vitatu tofauti iko wapi?na wasingetolewa mpaka leo wangekua na viporo kumi,lawama itupie tff na bodi ya ligi.
ReplyDeleteHoja za Yanga sio za msingi bali ni za mcenge. Hoja za Yanga kwakuwa wao hawakufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa waliotolewa mapema na Kwa aibu basi wanachoombea ni kuona Simba haifiki kokote ila kuna vitu vipo kwenye asili ya mtu, Simba na mashindano ya kimataifa wala usiwatakie mabaya unaweza ukapata ugonjwa wa moyo kwani ni kama vile wana zari nayo mara pa nusu fainali.
ReplyDeleteBongo tutasubiri sana,ndio mana tunafungwa hadi na sudani kanchi ambako soka lake liko nyuma sana,maendeleo hayaji kwakutengeneza makundi ambayo yatasababisha utengano na kuchochea chuki baina ya klabu moja na nyingine,chamsingi ni kukubaliana na hali halisi ya maendeleo ya soka letu,tmu inapopata bahati kushiriki kwenye michuano mikubwa kama hiyo lazima kuanzia nchi na vilabu lazima vikubali kwamba nchi yetu inawakilishwa na flani hivyo basi hatuna budi kutoa sapoti kwa namna yoyote ile ilmradi iweze kusonga mbele na ikiwezekana kuchukua ubingwa wa afrika.lengo kutangaza nchi kisoka.tuwe wazalendo jamani.
ReplyDeleteShida bongo timu kubwa yanga na simba kubebana kwingi, mnoo yaliyokuwa yanga sasa yamehamia simba, sheria ya FIFA mchezaji anaweza kucheza mechi kila baada ya masaa 72 na kuendelea, asa timu inamaliza wiki mbili imecheza mechi mbili, bongo lawama ni zile zile sema zinahama tu upande kwenda upande wa pili
ReplyDeleteHivi si ni juzi tu Yanga alikuwa anazidiwa idadi ya mechi na Simba na Azam...na zilikuwa zaidi ya mbili...Mbona Simba au Azam hawakulalamika.. Inaonekana Zahera anapenda sana kulalamika.Time table ya kwanza ilipotoka ilionyesha Yanga ilikuwa ianze mechi tatu nje ya Dar.. Zahera akacharuka.Alipopewa mechi zaidi ya kumi Dar ...akachekelea
ReplyDeleteKachinja john hiyo,angechinja ramdhani ingekua halali.mungu inusuru simba mungu ionyeshe mwanga timu yetu ya yanga.
ReplyDeleteKachinja john hiyo,angechinja ramdhani ingekua halali.mungu inusuru simba mungu ionyeshe mwanga timu yetu ya yanga.
ReplyDeletehayo yanga mwanzoni walilalamikia ratiba matokep yake wakapewa mechi kumi kuanzia nyumbani waache kulalamika wacheze mpira
ReplyDelete