TAKUKURU FANYIENI KAZI MADAI YA ZAHERA
KWA mara nyingine juzi Ijumaa mchana, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amerudia kauli yake ya tuhuma za rushwa kwenye Ligi Kuu Bara, anadai kuna timu kubwa inacheza mechi za timu nyingine.
Kocha huyo licha ya kwamba hakutaja jina la timu husika lakini alidai kuwa kuna klabu moja tajiri inayohonga marefa na wachezaji wa timu pinzani kwenye mechi dhidi ya Yanga.
Zahera amedai kuwa timu hiyo imekuwa ikitoa kiasi cha fedha kwa waamuzi na wachezaji katika mechi zinazoihusisha Yanga. Akaenda mbali zaidi kwa kutolea mfano mechi yao dhidi ya Singida na ile JKT Tanzania ambazo zote zimechezwa ugenini.
Amedai hadharani kuwa uongozi wa timu moja kubwa uliwaahidi wachezaji wa Singida Sh10milioni kama wangeifunga Yanga na Sh5milioni kama wakipata japo sare. Akaenda mbali zaidi kwa kudai kwamba hali kama hiyo ilitokea pia kwenye mechi na JKT Tanzania mjini Tanga.
Anadai kwamba wamepewa ushahidi na wachezaji wa timu hizo ambao baadhi yao waliwahi kuichezea Yanga katika misimu ya hivikaribuni na wana mapenzi na Yanga.
Maoni yetu sisi ni kwamba tuhuma za Zahera ni nzito sana na hazipaswi kupuuzwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania pamoja na kuhakikisha mambo yanakwenda kwa haki.
Rushwa ni kitu kibaya sana kama kikiruhusiwa kustawi kwenye soka letu haswa katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi hazina fedha.
Takukuru na TFF ni vyombo ambavyo vinapaswa kuyafanyia kazi kwa kina madai hayo ya Zahera na ikiwezekana hata yeye mwenyewe aitwe avisaidie vyombo husika kwa masilahi ya soka la Tanzania.
Siyo sahihi na wala haikubaliki kwenye soka klabu kuhonga waamuzi na wachezaji wa timu pinzani ili timu nyingine ifungwe.
Hiyo ni rushwa mbaya kabisa ambayo kila mwanamichezo anapaswa kuipiga vita ndio maana tunasisitiza kwamba vyombo husika viongeze umakini na viingie kazini kufanya kazi yao kukomesha hayo.
Kama ni kweli hali hiyo ikistawi itaua kabisa soka letu na kila mara tutakuwa tunapata wawakilishi feki kwavile ushindani hautakuwepo. Tuache soka lichezwe na kila mtu mwenye uwezo ashinde kwa haki uwanjani bila matumizi ya rushwa au mambo mengine mbadala.
Hali ya kupenyeza rushwa kwa waamuzi kutazinyima haki timu zingine na kufanya ligi yetu kupoteza mvuto kwavile baadhi ya timu ndizo zitakuwa zinatamba tu na kufanya zinavyotaka haswa kwenye wakati huu ambao mashindano hayo hayana mdhamini mkuu.
Tunakemea kwa nguvu rushwa michezo kwani kama ilivyo kwenye maeneo yote ni adui wa haki.
Tunavisisitiza vyombo husika kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na mamlaka za Serikali zitoe macho mawili kwenye Ligi yetu ili kuhakikisha madudu kama hayo yanatokomezwa.
Kila mmoja anapaswa kushinda au kushindwa kwa haki na si kwa shinikizo la mtu, kikundi au timu fulani yenye nguvu ya fedha.
Tanzania lazima tubadilishe fikra zetu na tucheze soka uwanjani. Madai ya Zahera yafanyiwe kazi kwa umakini yasipuuzwe au kuchukuliwa kama jambo jepesi.
Burden of proof anayo Zahera aitwe asaidie vyombo vinavyohusika .Kama ni kweli hatua zichukuliwe nä kama ni uzushi basi hatua kali zichukuliwe dhidi yake.
ReplyDeleteKulipa timu motisha ishinde nä kuhonga ili uachiwe ni viti viwili tofauti.
Kuna timu iliipa mchezaji Fey Toto aichezee Yanga kama zawadi na huku amaesaini hiyo timu.Fomu zikachanwa.
Timing ya madai haya inatia wasiwasi baada ya Yanga kupoteza pointi 10 katika pointi 15 ndio madai yamejirudia.
Kocha anadai wachezaji waliomwambia ni wachezaji waliowatoa kwa mkopo au waliowahi kuchezea Yanga.Awataje kwa vyombo vinavyohusika bila hivyo itakuwa uzushi na uchafuaji wa ligi.
Aweke ushahidi hadhalani ili madai yake yawe na tija, maana yeye kila timu iliyoleta upinzani kwake imepewa rushwa, i mean hata YANGA kufungwa na SIMBA uwenda kuna wachezaji waliopewa rushwa?
ReplyDeleteTimu Tajiri Kwa Sasa Ni Simba Na Azam Kati Ya Hizo Lazima Itakua Simba Kwanamna Azam Wanavyo Pata Matokeo Mabovu Zahera Asiachwe Bila Kutaja Watu Wanao Rudisha Nyuma Soka Letu Na Serikali Yetu Ina Pinga Rushwa Huyo Kocha Amezoea Uzush Anapo Shindwa Kushinda Na Ole Wake Akashindwe Mahakamani Afukuzwe Nchini Anachafua Ligi Na Nchi Yetu Na Simba Ili Ifunga Yanga Jana Ilipewa Rushwa Na Nani?
ReplyDeleteHatari nyingine ni kwamba anaongea vipi na wachezaji anaodai wana mapenzi na Yanga!!!!
ReplyDeleteTimu zingine zikidai ana wa influence ili waseme au wafanye anachotaka yeye utakuwaje?
Natilia shaka sana professionalism ya Zahera kwenye stress.
Madai kama haya yanaweza kumwingiza kwenye matatizo makubwa.
Inabidi abanwe watoe ushahidi haraka iwezekanavyo. TFF na bodi ya ligi mwiiteni mumuhoji.
Kocha huyu alidai muda mrefu kwamba kuna njama TFF ikakaa kimya!!!!
ReplyDeleteWakiongea wengine wanaitwa watoe ushahidi!!
Kwa nini yeye awe immune?
Kweli Kabisa Huyu Zahera Nina Wasiwasi Na Kaul Yake Na Sikitika Haja Taja Timu Ila Nina Uwakika Alikuwa Ana Ilenga Simba Maana Ndo Timu Inayo Ongoza Kwa Posho Kubwa Kwa Wachezaji Mbali Na Mishara Tunaomba TFF Imubane Kocha Huyu Ataje Viongozi Wanao Toa Rushwa Marefarii Na Wachezaji Wanaopokea Rushwa Maana Ni Kosa Kutoa Na Kupokea Rushwa Sasa Tuone Hawo Wachezaji Wanye Panzi Na Yanga Kitakacho Wakuta Itakua Kama Mchezaji Mmoja Wa Zamani Wa Timu Ya Taifa Kenya Mpaka Sasa Anakesi Na Fifa Tuhuma Kama Hizo
ReplyDeleteZahera Atambue Ni Mambo Makubwa Hayo Na Akikosa Ushahidi Yata Mu Cost
Hiyo ni kocha ni kichaa..anachezea Moira kwenye vyombo vya habari!So akaende Takukuru
DeleteKamata Zahera sukuma ndani akatoe ushahidi
ReplyDeleteZAHERA AHOJIWE NA TAKUKURU ASITAKE KUCHAFUA WENZIE BILA USHAHIDI YEYE ATOE USHAHIDI
ReplyDeleteKichaa huyu...eti kuna timu inacheza mechi za Yanga..Akishinda hiyo timu haijatoa hela.Akitoa safe hiyo timu inahusika...Vipi na Jana hiyo timu imehusika
ReplyDeleteMahusiano haya ya kocha na wachezaji wa timu pinzani anayocheza nayo kuwasiliana na kupeana mawazo ya kuisaidia Yanga , yeye anaona ni sawa?.kaongea kasahau kwema nukta. Siri zote nje
ReplyDeleteYea, yea, .... Yanga hutumia wachezaji wanaopeleka timu kwa mkopo katika Upanga matokeo na si vinginevyo. Hiyo ni rush a kama rush à nyingine.
DeleteWachezaji wote wa Amani wa mayebo wapelekwe ndani ni à mahojiano na TAKUKURU.
Kocha BWEGE sana Zahera, sijui anakula nini.
Mtatukana sana Ila ukweli ligi imejaa rushwa tu
ReplyDeleteHapa ukweli utaonekana uongo kisa hamsa hamsa waonekane wakweli
Angalia hata idadi ya viporo yote hyo ni upangali wa matoke
Povu ruksa na nguo chafu✋✋
why always zahera?
ReplyDeleteLeteni ushahidi. Sio mambo yameanza kuwa magumu mnaanza uzushi.Mmepoteza pointi 10 kwenye mechi 5 kelele zimeanza.
ReplyDeleteMngekuwa mnajiamini msinge paki basi. Mnacheza na walinzi 8 .Chezeni mpira. Formula ya kutojiamini ndio imefanya Mourinho amekuwa failure.
ReplyDeleteCheza mpira.
Hata Simba waliwahonga wachezaji wa Alahly wawaachie na kufanya timu yao kupoteza mechi? Hata wachezaji wa Azam Fc wanahongwa na timu nyengine ligi kuu ili timu yao isifanye vizuri? Kama kuna timu tajiri inatoa fungu lake la pesa kwa timu nyonge ili kuwapa motisha wachezaji wao kutoa ushindani kwenye ligi kuu basi hiyo timu ni ya kupongezwa na wala sio rushwa hata kidogo. Labda suala la kuhongwa waamuzi na sidhani kama Zahera anauhakika na anachokiasema kwani kitakwimu Simba ni muathirika mkubwa kama si namba moja wa maamuzi mabovu ya waamuzi kwenye ligi kuu sasa utaona tuhuma za Zahera na Yanga ni kutokana na kuwa tayari walishakuwa na matokeo yao vichwani yakwamba wao watakuwa mabingwa na watashinda mechi zao zote hata ile ya wapizani wake wa jadi. Zahera kwa kawaida huwa anaropoka vitu vingi na si busara kila anachosema kikachukuliwa kuwa ni kweli inaonekana hana matumizi mazuri ya mdomo wake. Mfano mechi ya jana kati ya timu yake ya Yanga na simba goli lile alilofungwa Dogo kabwili kama angelikuwa kakolanya asingefungwa amini usiamini ila ni maamuzi ya Zahera. Sasa anataka kuwaaminisha watu vitu vingine vya ajabu wakati moja ya tatizo la Yanga ni kipa.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteNi kweli na wala sio siri simba huwaahidi na kuwapa fedha wachezaji wake ili washinde mechi zao . kama ni rushwa , ingekuwa timu inapewa ili ishindwe kama walivyopewa wachezaji wa yanga , lakini siyo ipewe ili imshinde yanga . kama ni rahisi kihivyo yanga waje kwangu nitawapa bilioni mia moja ili wazipe timu zote ligi kuu ili ziifunge simba . tuache masihahara , zahera kamata weka ndani
ReplyDeleteZahera ana ugonjwa wa kulalamika..Ratiba ya kwanza kuanza ligi ilipotolewa Yanga ilikuwa ianze ugenini michezo 3..Akalalamika ndiyo akapewa ratiba ya kuchezea mechi za kwanza zaidi ya dazeni Dar.Baada ya halo akaanza viporo eti ratiba inapendelea Simba..Kwenye vyombo vya habari anauliza wiki hii hapa katikati Simba ana mechi yeyote?Ni kwa nini?Wakati Simba siku chache ilikuwa icheze na Nkana..Akajitoa Mapinduzi eti ratiba inabana timu ikapata mapumziko wakati Simba wakatumia Mapinduzi Cup kujiandaa na mechi JS Soura.Akenda kwa Stendi akavurunda na Sportpes hakupata hata zawadi yeyote..Tangia hapo ni kwamba ligi sio makini na ubingwa utakuwa sio halalali..Hizi hujuma sio Mpya mwaka juzi wakati Malinzi na Mwesigye wamewafanyia figisu Simba hadi akapoteza ubingwa..Kagera Sugar wamechezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano..Simba wamekata rufaa...TFF wakaitupilia mbali rufaa eti imewakilishwa bila malipo...Swala LA kadi tatu hawakuliongelea kabisa..Kwa Malinzi na Mwesigye Kagera Sugar ya huko kwao Kagera haikufanya kosa na kama ingrpokwa point ubingwa angekuwa Simba!Yanga wajue hata kama wao sio ubingwa halali mwaka huu walishafanya figisu za kuchukua ubingwa toka kwa Simba mwaka juzi!
ReplyDeleteTFF wenyewe wamechangia sana hizi hisia kuibuka.. Kwanza Ligi Kuu haina mdhamini.. Unategemea nini kwa zile timu ambazo zinapata wakati mgumu kuweka kambi, kusafiri hapa na pale na gharama nyingine za maandalizi..!!??
ReplyDeletePili ubovu wa ratiba ya Ligi Kuu... Kuna timu zipo hapa hapa nchini lakini hawajawahi kutana si kwa raundi ya kwanza wala ya pili..
Tatu kuna timu ina viporo vya raundi ya kwanza wakati wenzao wakiwa mechi kadhaa za raundi ya pili..??!!
Ni wazi kuwa timu iliyojipanga vizuri ikianza kupasha na kushinda viporo vyake ni lazima hisia za rushwa zitajitokeza..
Ila sasa chanzo cha tuhuma za rushwa pia kinatia mashaka makubwa.. It is not a balanced source.. It is definitely biased!!
Naungana na wote wanaodai huyu kocha aitwe ili kuthibitisha madai yake.. Uchunguzi ufanyike.. Na matokeo ya uchunguzi yashughulikiwe kikamilifu..!!
Saleh Ali wewe ndio umeleta hiyo habari. Ungekuwa mwandishi mwenye weledi unge balance stori kwa kutuliza ushahidi au hata kuwahoji TFF!!!
ReplyDeleteHii mimi naona ni agenda ya kutafuta sympathy.
Saleh Ali call a spade a spade and show your guts as a reporter.
Saleh Jembe Mara zote habari sake huwa zimeelemea upande mmoja.Sio wastaarabu kabisa..na ukifuatilia habari zao utajua kwamba wao ni Yanga.Mfano Kagere alipofunga bao dhidi ya All Ahly kwenye live update ya dakika baada ya dakika...Waliandika tu Kagere amefunga bao zuri..Nina hakika ingekuwa ni Yanga wanmefunga wangeaandika neno Gooooooooliiii.Lakini kwa kuwa ni simba roho iliwauma kushangilia.
ReplyDeleteTurudi kwa Zahera ni vena atumie busara kama za babu wa Azamu Prujim ambaye amesema kutokufanya vizuri timu yake ni upepo mbaya tu ambao utapita..Anapaniki kwa kuwa katika mechi tano zilizopita keshapoteza point 10...Sasa lawama Mara Ratiba, Mara waamuzi, Mara viwanja, Mara timu zingine zinapendelewa..Mara sasa rushwa..Aitwe kamati ya maadili ajibu na afafanue hizo shutuma zake
Na kwa akili yake na busara sake kabisa Salehe anaandika Takukuru fanyieni kazi malalamiko ya Zahera..Basis kama mnaona malalamiko ya Zahera yana ukweli na siyo ya MFA maji anayetapatapa basis yachukueni nyie wenyewe myapeleke Takukuru...Nyiye si ni vibaraka wa Yanga!Nendeni wenyewe Takukuru!
ReplyDeleteAjibu sio kwamba alishindwa kwa kudhibitiwa na Zana..labda kufutaba na akili finyu...bichwa maji ya Zahera ni kuwa naye atakuwa alipewa rushwa na viongozi wa timu tajiri!
ReplyDeleteHuyo Ajibu alifurukuta lini kwenye mechi ya Simba?
ReplyDeleteMechi iliyopita alitolewa.
Hili halijaanza leo, imekuwa ni kawaida kabisa kwa timu kuhonga timu pinzani au marefa. TFF wamekaa kimya kwa sababu wanajua vilabu hivyohivyo ndivyo vinavyowaingizia pesa na wao wamekuwa sehemu ya hiyo rushwa.
ReplyDelete