June 1, 2018


Beki Mtanzania anayekipiga katika Klabu ya Baroka ya Afrika Kusini, Abdi Banda, ameweka bayana kwamba hadi sasa ana ofa za timu 15 ambazo zinahitaji saini yake baada ya kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza nchini Afrika Kusini.
        
Banda amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Baroka FC kwa msimu uliomalizika hivi karibuni wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), ambapo amechangia kwa kiasi kikubwa kuibakisha timu hiyo isishuke daraja.

Beki huyo ndani ya msimu wake wa kwanza akiwa huko amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 39 za michuano yote kwa timu hiyo na alichaguliwa mara mbili kuwa mchezaji bora wa timu yake wa mwezi.

Banda amesema timu hizo ni za kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini ambazo zinamhitaji baada ya kuonyesha uwezo ndani ya kikosi chake cha Baroka alichojiunga nacho akitokea Simba.

“Hadi sasa kuna timu 15, ambazo zimeonyesha nia ya kunihitaji kwa ajili ya kuzichezea kwa msimu ujao, ambapo mambo yote yanasimamiwa na wakala wangu ambaye ndiye msimamizi wa kila kitu kwangu.

“Zote hizo zimekuja kwa sasa baada ya kuonyesha uwezo nikiwa Baroka FC, ikizingatiwa huu ndiyo kwanza msimu wangu wa kwanza kucheza katika ligi na timu hiyo,” alisema Banda.

Wakala wa Banda, Paul Mitchell, kutoka Kampuni ya Siyavuma Sports Group, alisema: “Banda ni mchezaji mzuri na amekuwa na kiwango kikubwa katika msimu wake wa kwanza akiwa hapa. Ni kweli kuna timu ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka kwa ajili ya msimu ujao lakini kwa sasa siwezi kusema ni timu gani hizo.”

CHANZO: CHAMPIONI

7 COMMENTS:

  1. Kama zipo ofa hizo 15 ni zake yeye mwenyewe achague moja aende huko. Kututangazia hapa ni kutaka sifa tu zisizo na maana. Banda awe na ofa 15. Chirwa na Okwi watakuwa na ngapi?

    ReplyDelete
  2. Huyu Banda angefikia angalu nusu ya thamani ya Samatta sijui ingekuaje. Kiwango cha kawaida sana lkn haishi kujisifu kwenye media.

    Kuna Siku aliwahi kusema hamna mchezaji yeyote wa Simba na Yanga anayeweza kumfikia kwa malipo anayolipwa. Unasema haya ili iweje? Tokea aondoke Simba hajawahi kuongea neno zuri kuhusu Simba ambao wamemlea na kumfikisha alipo.

    Angalau msuva anaonyesha shukrani kwa Yanga kuwa imemfikisha alipo na kila akirudi anawapa sapoti na kwenda uwanjani kuwaona. Kijana Banda jirekebishe usituletee mipasho ya Tanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mchezaji hafai. Ana tabia ya kujiona na kujisikia.Hana mpira wowote wa kujigamba hivyo ila ni hulka yake tu mbovu.

      Delete
  3. Majani ya south si mchezo

    ReplyDelete
  4. usifanye uchoyo basi kati ya hizo ofa wapatie na kina Ajibu,MO Ibrahim,Himid Mao tupate kuongenza watanzania wanaocheza nje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hana lolote hizo ofa 15 za mdomoni au maandishi? Aziweke mtandaoni tuzisome ili tuhakikishe maana mtoto huyu ni misifa tu . Ona mwenzie Himid Mao kasepa Misri kwa heshima zote hana majivuno masikini kijana huyu mstaarabu kweli Mao safi sana.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic