August 20, 2020

 


UONGOZI wa Yanga, rasmi leo umemtambulisha Senzo Mbatha kuwa mfanyakazi wao ndani ya klabu hiyo akitokea Klabu ya Simba.


Senzo alijiuzulu nafasi yake ndani ya Simba hivi karibuni na kuzua mshtuko mkubwa kwa wanachama na viongozi wa klabu yake ya zamani kwa kuwa hawakujua anaweza kuibukia kwa watani zao wa jadi.


Akiwa ndani ya Simba, Senzo aliweza kuiongoza Simba kwa mafanikio makubwa na kusimamia usajili wa mchezaji wao nyota Luis Miqussone ambaye inaelezwa kuwa alikuwa kwenye hatua za mwisho kuibukia Yanga.

Sababu kubwa ya Senzo kusepa ndani ya Simba inaelezwa kuwa mkataba wake ulikwisha na mabosi wa Simba waligoma kumuongezea mkataba mwingine jambo lililomfanya bosi huyo abagwe manyanga kabla ya muda wake kuisha jumlajumla kwenye mkataba wake.


Leo, Agosti 20, Yanga wamemkaribisha kiongozi huyo Jangwani  rasmi ndani ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inaboresha kikosi chake.

7 COMMENTS:

  1. Alipojiona karibu ya kutemwa haraka akaandika kujiuzulu na Gongonje haraka wakajiokotea wakijinata eti Mnyama hawawezi

    ReplyDelete
  2. Kwani alianZia Simba,mbona anayemlipa kanyamaza maisha yaendeleee?

    ReplyDelete
  3. Huyu salehe ni mrangi au nyaturu..
    Bogas kabisa

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni Team majungu Mimi nakumbuka Okwi alipo hama kwao walisema ana ukimwi tena hiyo habari mimi niliambiwa na Kiongozi wao tena mkubwa so hawa kila Mtu akishindwana nao always ni kumnanga

    ReplyDelete
  5. Angalia hata Makocha wanawabeza likewise

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic