November 19, 2020


SUALA la mabadiliko ndani ya Simba limeleta sura mpya baada ya Serikali kujibu mapigo ya viongozi wa timu hiyo ambao waliweka wazi kwamba wanakwamishwa na Serikali.

Simba kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kuelekea kwenye mabadiliko ambao bado haijakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa timu hiyo kushindwa kukamilisha taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 19 imeeleza namna hii:-


21 COMMENTS:

  1. Kwa mawazo yangu; tume inatakiwa kufanya kazi na taarifa za mezani sio za kwenye media na vyombo vua habari.
    Kama Kuna taarifa zipo mezani halafu mnasitisha mchakato kisa mitandao ya kijamii imesema nini sijui, huo ni ushabiki sio weledi hata kidogo.

    Let's work professionally guys!

    ReplyDelete
  2. Hawa wanazingua Kama simba kunavipengele haijanalizia mbona walikuwa hawavisemi siku zote, mpaka viongozi wasimba waanze kutoa kawama ndo wanataka masuala hayo ya ipengele. Hawa jamaa hawataki Simba isonge mbele kwakupiga hatua za maendeleo

    ReplyDelete
  3. Hii tume kama kweli ni ya serikali halafu inaliweka shauri moto kabisa kama hili la mabadiliko ndani ya simba tena ni la uwekezaji kwa miaka mitatu basi ni hatari. Fikiria kama Mo angekuwa mgeni unafirkiri bado angekuwa na hamu na kuendelea na mchakato huo? Ushindani gani au Mshindani gani anaengojewa kushindana na Mo kuekeza pale simba kwa miaka mitatu? Mambo mengine sisi kama watanzania ni hovyo kabisa. Ni juzi tu tumetoka kulia na matokeo ya Taifa stars zidi ya Tunisia halafu tunamtafuta nchawi? Mpira unahitaji uwekezaji sio blah blah blah. Vilabu vya Tunisia kama Esperence na vinginevyo ni washindani wa mashindano makubwa ya Africa na sio washiriki kama timu zetu na huko wachezaji wao wanapata uzoefu na kuonekana nakupata masoko ya kununuliwa. Lakini Vipi wamefika huko? ni uwekezaji tu unaowaezehsa kugharamia academy za kulea vijana katika misingi sahihi ya soka. Suala la uwekezaji ndani ya simba kwakweli linasikitisha na taasisi inaolishughulukia inapaswa kuchunguzwa kwa Rushwa.Na kama sheria zetu ndio inavyoelekeza kukaa kimya na shauri la uwekezaji kwa zaidi ya miaka mitatu wakishughulikia suala moja la simba bila kupata jawabu basi sheria zetu zinatujengea mazingira ya kutumaza kimaendeleo ni hatari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka tatizo sio serikali tatizo ni vilabu havijaweka mambo yao sawa

      Delete
    2. KUNA MTU ANA HELA ZA KUCHEZEA, ILA ANAPOTEZA MUDA WAKE. KWA BAHATI MBAYA MO KAZALIWA KAMA SIMBA NA ATAKUFA KAMA SIMBA. SASA HUYO ANAYEJIPENDEKEZA SHAURI YAKE. KUNA WATU HAPO WASHAKUFA KISA SIMBA HIYO HIYO

      Delete
  4. Kwani Simba haina wataalam wa sheria wenye kujua nini kinatakiwa?Kuna watu wamelipwa kuhakikisha mchakato unakamilika kulingana na kanuni na taratibu za kisheria na sio kazi ya tume kuwafundisha nini cha kufanya

    ReplyDelete
  5. Mbona barua ya tume imefafanua vizuri tu mawasiliano iliyokuwa ikifanya na Simba kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia na kupewa miongozo ya nini cha kufanya ila utekelezaji ukawa haupo sasa mlitaka tume ijigeuze na iwe ni uongozi wa Simba ifanye maagizo iliyoyatoa kwa uongozi wa Simba
    Hebu someni hiyo barua kipengele kwa kipengele then mtapata majibu tosha na kugundua madhaifu ya uongozi katika kukamilisha maagizo waliyokuwa wanaelekezwa

    ReplyDelete
  6. Hata kama katiba iliyopitishwa inatamka kuwepo na bodi ya wakurugenzi....lakini wakati huo huo mabadiliko yawe yameshamalizika ambapo inaleta legitimacy ya kuwepo bodi ya wakurugenzi ya Kampuni iliyopitishwa na Kuanza kufanya kazi kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya Simba....Shida ni kwamba, hata mabadiliko ya muundo wa kuwa na kampuni itakayoitwa Simba Sports Club (Kampuni Tanzu/Muungano wa Simba Sports Holding Co & Mo Simba Sports Ltd) hayajapitishwa Bodi imeshaundwa na CEO ameteuliwa.....hapo ndipo kuna mushkeli....ilitakiwa Simba Sc Club iunde Kamati ya Mpito kuongoza Klabu hadi hapo mabadiliko yatakapo kamilika halafu sasa waunde bodi ya wakurugenzi ya itakayokuwa Simba Sports Club Ltd (Joint Venture between Mo Simba Sports Club & Simba Sports Holding Company-ambazo zote zinaleta maswali ya uhalali wao na uwepo wao)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka umejitahidi kufafanua vizuri kulingana na maelekezo kama yalivyotolewa na tume,Tatizo letu Watanzania huwa tunakurupuka kujibu au kutoa shutuma bila kusoma nini kimeandikwa au kimetolewa kutolewa ufafanuzi.Wanaoishutumu tume wapitie kipengele kimoja baada ya kingine ndipo watakapoelewa jinsi FCC ilivyokuwa inatoa miongozo.Tatizo tulishazoea njia za mkato lakini sasa hivi ni mwendo wa kunyooka

      Delete
    2. INAWEZEKANA KUWA MUONGOZO UPO SAHIHI LAKINI SIO KINACHOOTENDWA NA OFISI HUSIKA. CHUNGUZENI MTAGUNDUA. KWANINI SIMBA IMEWWEZA KUBADILI VITU VINGI VYA KIUTAWALA? MBONA HAPO AWALI HAIKUWA HIVYO? KUNA WATU WANA JAMBO LAO

      Delete
  7. Viongozi wa Simba wakamilishe utaratibu, wasitafute mchawi...

    ReplyDelete
  8. Tume inanuka rushwa kwani longo longo zote hizo za nini kisa tu mtu anatakuekeza, kutengeneza ajira,kulipaisha jina la Tanzania kimataifa,kuinua vipaji halisi vya soka vya kitanzania,hapa kiuhalisia anaecheleshwa sio Mo au simba tunajichelewesha sisi wenywe watanzania taasisi zetu nyingi zimejaa ubabaishaji na rushwa ila mazumwamwa pekee ndio watakaosapoti kasi ya utendaji wa kazi wa mwendo wa konokoko.

    ReplyDelete
  9. Hapo tu wewe unayeshutumu tume kwa rushwa ,hujatambua kuwa kwa taarifa ya tume tayari Mo na mchakato wake na Simba pana dalili za rushwa? ,labda hujui maana ya rushwa.Halafu ku kataa uadilifu kisa kutangaza nchi huo Ni ufinyu wa fikra na ushetani kwanini hafati taratibu?.Unasema Viongozi sijui nchi yet huyo Mo katokea Canada?si alikuwa mbunge wa Singida au ulikuwa hujazaliwa.Please hayo Ni marekebisho Madogo atii/mtii mmalize game.

    ReplyDelete
  10. Halafu Uwekezaji wa huyo Bwana wewe unaouona una tija ni kwa matakwa yako kama mpenzi wa Simba bt not kwa Tanzania ,na viashiria hivyo ni pamoja na jamaa kuomba aongezewe Wachezaji watano wa nje kisa eti atangaze nchi ,Sasa hapo ukiangalia kinachoendelea Kuna kusaidia Tz au matakwa ya Mo cse anataka kuajili foreigner ,niliuliza issue ya Ilanfya mlikaaa kimya,na mwisho Simba iliyocheza final na Stella ilikuwa na foreigners wangapi na je Tz vs Tunisia Tz ilikuwa na Wachezaji wangapi Wanacheza Ligi za Ulaya?mbona tumeona improvement why not Mo kuwekeza kwa Wachezaji wa ndani?

    ReplyDelete
  11. Tatizo wanachama wa simba wamekuwa kama vipofu, hawaelewi kila jambo lina utaratibu wake . kingia kwenye mfumo ni sawa na kujilipua kama hukuelewa, utakuja kuelewa ullingizwa mkenge baada ya miaka 10 ijayo. kila jambo nchi linafanyika kwa mujibu wa sheria. katiba yako iliyoandikwa bila kujua ya mbele irudie kuisoma. haiwezi kuifanya serikali kufanya kazi yao kwa manufaa ya wengi. Angalieni maslahi ya wengi sio ya mtu mmoja. anawadanganya kwa viela vidogo lakini mwenzenu ana malengo. Atawabana katika sehemu chache na timu itakuwa mali yake. Ukijafunguka tayari umechelewa. Fuateni ushauri wa watalaamu wa FCC na mmalize mchakato. Hakuja jambo lisilokuwa na kufuata sheria. Ukiona mtu na kundi lake wanataka mambo ya haraka bila kutoa documents muhimu ujue kuna jambo linafinchwa ili kuwahadaa wengine wasioelewa. kinachooendelea. Timu itataliwa na familia ya mtu mmoja na wapambe wake wanaofaidi vipesa wanavyopewa kwa njaa zao. Mwenyekiti wa simu akijiuzulu kwa kuwa aliona mbali. Kingwangala alihoji kwa kuwa ameshaona mbali. Nyie wengine bado usoni mna giza nene. fungueni macho ili kika kitu kiwe wazi. HARAKA HARAK HAINA BARAKA NA POLE POLE NDIYO MWENDO WENYE MAFANIKIO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona hoja yako ni kama unajipinga mwenyewe ni sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe.Umesema wanasimba wanatakiwa kufanya huu mchakato sio Kwa mihemko na kumbuka kila wakati viongozi wa Simba wamekuwa wakieleza Kwa uwazi kuwa mchakato uko Kwa FCC hivyo MO hawezi kuweka 20b sababu ya kusubiria kitakachoamuliwa na FCC.Lkn hapo hapo unawapongenza Hamis Kigwangala na Nkwabi Kwa kuona mbali na hapo sijui unawasifu kitu gani?Wakati wao ndio wanaotaka 20b iwekwe tu bila ya kufuatwa taratibu husika kama michakato hiyo kupitia FCC..Je MO ni kipofu au mwendawazimu asiyeijua 20b?Je FCC ni wapumbavu kuwaambia bado kuna kasoro ktk kukamilisha mchakato wa mabadiliko? Je FCC ikisema vigezo na masharti havijakidhi kuingia kwenye soko la hisa la ushindani na MO akarudi Kwa wanachama waliompa ridhaa ya kumiliki hisa 49% na kuwaambia FCC imetupilia mbali ombi letu hivyo naondoa kusudio langu la kumiliki hisa 49%...Je tutarudi Kwa Hamisi Kigwangala na Nkwabi, Kilomoni kuwaomba watutafutie muwekazaji au ndio tuanze mchakato wa kutembenza bakuli...kama ilivyo watokea Yanga na Manji.

      Delete
  12. Msifikiri yale MO anayoyafanya kwa simba yeye ni mjinga, mwenzenu anaweka rekodi zake sawa na kila gharama anaijua na mjue kila pesa anayotoa nje ya ubia innandikwa na kama hamjui kuna mtu ndani ya timu anasaini kwa niaba ya simba. ikitokea la kutokea mtaletewa bill kubwa ya deni ili klabu ilirudishe pesa zake . kulipa mishahara, kujenga uwanja na mengine mengi najua wanachama hamyajui mtakuja kuulizana , kwani anatudai? usipende dezo kupata vya bure ukiwa ni masikini na huna njia mbadala ya kupata kipato. MO kaja juzi tu kuna watu wanaijua simba kuliko nyie kizazi cha tamaaa na kupenda vya bure. lakini hao waliohangaika na simba mpaka MO anafurahia kuimeza wanatukanwa na kupigwa mateke kisa hawana pesa. MTAKUJA KUJUTA HUKO MBELE. WENZENU YANGA KWA KUWA NYIE MNAJICHANGANYA WANAJIFUNZA JAMBO NA HUENDA MCHAKATO WAO UKAFANYIKA KITAAALAMU NA KUFANIKIWA KABLA YENU. KWA KUWA WENZENU NI WASOMI ZAIDI YENU. KAENI CHINI MTULIE KILA KITU KIWE WAZI HATUA KWA HATUA. MSIJE INGIA MKENGE. KUMBUKA SIMBA SIO KAMA AZAM. KAMA MO ANA PESA SI AANZISHE KLABU YAKE AMBAYO HAINA MLOLONGO MWINGI? ANAG'ANG'ANIA NINI SIMBA? NA KWA NINI AWE MWEKEZAJI PEKEE.?KUNA JAMBO NYUMA YA PAZIA. MBONA BAHRESA NI SIMBA LAKINI ANA TIMU YAKE. AANZISHE "MO FOOTBALL CLUB" NA HUKU AKIENDELEA KUISAPOTI SIMBA KAMA MWANACHAMA TU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanachama wa Simba waliridhia MO achukue hisa 49% na hisa 51% zibaki Kwa wanachama.Ni wanachama wa Simba ndio wanaweza kuamua kwa ridhaa yao kuwa hatumtaki MO kuwa mwekezaji ndani ya Simba.
      Kumbuka kuwa mabadiliko haya ya Simba yana baraka zite za serikali.Tatizo ukute hiyo FCC imesha inginza siasa za usimba na uyanga

      Delete
  13. AnonymousNovember 20, 2020 at 8:26 AM
    Wenye hiyo taasisi baada ya kuona Mo kaenda kukutana na wabunge wanaonekana kuanza kuweweseka.Lengo la kucheleweshwa shauri la simba sio kutafuta mshindani wa uwekezaji au uteuzi wa CEO mpya ndani ya simba bali lengo lilikuwa ni kuizuia simba kufanya mabadiliko ya kimaendeleo nadhani kwa manufaa ya wala rushwa fulani wakati wanachama wenyewe wa simba walisharidhia mabadiliko ya kuitawala ndani ya klabu yao.

    Reply

    shaibuNovember 20, 2020 at 10:14 AM
    KUNA MKONO WA MTU HAPO, ILA BAHATI MBAYA HUYO MTU ANAPOTEZA MUDA WAKE, SERIKALI NA SHERIA ZA MPIRA HAVIENDANI

    Reply

    Anonymous November 20, 2020 at 3:33 PM

    Nafikiri MO amefanya vizuri kufikisha ujumbe huo kupitia Kwa wabunge.Imeshakuwa kero Kwa MO kila kukicha anaulizwa mzigo ataweka lini na kuonekana kama uwekezaji wake ni fake.Ni swala la kujiuliza kulikoni leo hawo FCC watoe waraka wao huo haraka hivyo baada ya MO kuwajulisha wabunge wanaoshabikia Simba kuhusu mchakato ulipokwamia? Kwa nini FCC hawajawahi kutoa tamko kujibu kuhusu mchakato ulipokwamia kama waliyowahi kutolewa huko nyuma na MO na pia wakurugenzi wenzake kwenye bodi ya kuwa mchakato umekwamia FCC?..Tumewasikia kina Magori, Mulamu Nghambi, Kaduguda,CEO Barbara na pia Haji Manara wakitueleza mchakato unasubiria maaumuzi ya FCC.Ingawa sina jawabu Kwa asilimia mia lakini nahisi kuna jambo lilojificha ndani ya FCC.Ndio mambo kama haya ya ukiriktimba ktk uwekezaji yamemfanya muheshimiwa Rais wetu Magufuli kuhamishia kitengo cha uwezekaji kwenda Ikulu.Issue ya kutekelezwa ndani ya mwezi mmoja inapeleka kuchukua miaka mitatu.Tujitathimini kwa kuzingatia kuwa Tanzania Kwa sasa imeingia kwenye uchumi wa kati.

    ReplyDelete
  14. Kwani wewe Wabunge wao si ni Kama Chigwangalla Mo kifupi mssaaaniiii tumalize hojaaaas

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic