Kwa
mara ya kwanza mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunguka
kuhusiana na uhusiano wake na Lionel Messi na kusema anamheshimu hasa juhudi
zake za kutaka mafanikio kama mchezaji pamoja na klabu yake ya Barcelona.
SWALI. Baada ya miaka mitano sasa na Real Madrid, umechoka
kulinganishwa na Messi au umejifunza jambo?
JIBU. Ni sehemu ya kazi tu kama vile ambavyo kwenye mashindano ya
langalanga (Formula 1), watu wanafananisha kati ya Ferrari na Mercedes. Haya
yamekuwa maisha yangu hapa Madrid, lakini najua mambo yanabadilika na hata
nilipokwenda Manchester kulikuwa na mengine tofauti.
SWALI. Kumekuwa na taarifa kwamba uhusiano wako wewe na Messi
nje ya mpira umekuwa si mzuri?
JIBU. Si kweli, sisi ni marafiki, ni marafiki kazini. Binafsi sina
rafiki nje ya mpira, pia sina urafiki na Messi nje ya mpira. Anajitahidi
kufanya makubwa katika klabu yake na timu ya taifa, sawa ninavyofanya mimi. Tunachezea
timu zenye upinzani mkubwa na huenda ushindani huo unafanya watu wayakuze hayo
mambo.
SWALI. Unafikiri wewe na Messi, siku moja mtakutana, mkae na
kuanza kujadili haya yaliyotokea huku mkiangua vicheko kwa furaha?
JIBU. Nafikiri inawezekana, soka ni
mchezo wa furaha, soka ni kitu kikubwa na unaweza kuufananisha na saa. Ndiyo
maana nashauri kuwaangalia wapinzani kwa jicho la mafanikio na kukubali
wanachofanya kwa vile ni kitu kizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment