September 22, 2014

DK SUFIANI (KULIA) AKIPAMBANA NA SHABIKI HUYO ALIYETOA MANENO YA KEJELI...

Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, uvumilivu ulimshinda hadi kufikia kutaka kuzichapa kavukavu na shabiki.
Sufiani ambaye alikuwa akisumbuka kuliingiza boksi zito la vifaa vya tiba pamoja na maji kwenye basi la Yanga, alishindwa kujizuia na kutaka kuzichapa na shabiki huyo wa Yanga, dakika chache baada ya timu hiyo kupoteza mechi yake ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.
AKIMSHUGHULIKIA SHABIKI HUYO...

Yanga ilifungwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri na shabiki huyo alitupa maneno ya kejeli akidai ana uchungu wa Yanga kufungwa.
Sufiani alijaribu kumsihi, lakini baadaye alishindwa kujizuia na kuamua kupambana nae.
Hata hivyo, mmoja wa mashabiki maarufu wa Yanga alijitokeza na kumzuia.

“Muache nimfunze adabu kenge huyu, hanijui kama mimi ni mtoto wa mjini kuliko yeye, muache kwanza nimpe vitasa vingine, hawezi kutuletea dharau zake za kilevi hapa, kwani nani anayefurahia kufungwa hapa?” alisema Dk Sufiani akionyesha kuwa na hasira.
AKIAMULIWA...

Sufiani alionyesha kukerwa na maneno ya shombo ya shabiki huyo aliyekuwa na hasira ya Yanga kufungwa katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic