Uongozi wa Mbeya City ya jijini Mbeya,
umefunguka kuwa upo katika mchakato wa kusambaza upya jezi zake baada ya
kuachana na zile za zamani kwa kufungua maduka mawili jijini Dar.
Mbeya City ina mpango wa kubadili jezi zake za
awali kutokana na kutaka kuweka nembo ya mdhamini mpya Bin Slum na kuachana na
zile za awali.
Katibu Mkuu
wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha
mchakato wa usambazaji wa jezi mpya ambapo watasaka mawakala wa kuwasaidia kazi
hiyo.
“Tupo katika mikakati ya kubadili jezi zetu
ambapo zitauzwa katika maduka mawili jijini Dar, moja lipo maeneo ya Sinza na
lingine litakuwa katikati ya mji, Posta.
“Tunawatafuta mawakala ambao watasimamia kazi hiyo
kwa kuhakikisha tunadhibiti hali ya watu wengine kuuza jezi hizo na hatua kali
zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayehusika na utoaji wa jezi zetu bila ruhusa,”
alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment