Mshambuliaji wa kimataifa wa Azam FC, Mrundi,
Didier Kavumbagu, ametamba kuwa sasa atahakikisha anafunga kila mechi ili
kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa.
Kavumbagu ameianza Ligi Kuu Bara kwa mkwara
baada ya kufunga mabao manne katika michezo miwili ya awali. Kila mchezo
akitupia mawilimawili.
Akizungumza na Championi Jumatatu baada ya
kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting
juzi kwenye Uwanja wa Chamazi, Kavumbagu alisema anafurahi kuona amekuwa katika
wakati mzuri ndani ya kikosi hicho lakini akasisitiza kuwa ataendelea kufunga
kila anapopata nafasi.
“Cha msingi ni kufunga tu, hilo ndilo suala
pekee linaloipa timu mafanikio, kwa hiyo nitajitahidi kufunga katika kila mechi
kadiri ninavyopata nafasi ili kuhakikisha naisaidia timu katika mbio za kutwaa
ubingwa, kisha hayo mambo ya ufungaji bora yatakuwa baadaye,” alisema Kavumbagu,
mchezaji wa zamani wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment