| NYOSSO (KUSHOTO) WAKATI AKIITUMIKIA COASTAL. KULIA NI DAVID LUHENDE ALIYEKUWA YANGA, SASA YUKO MTIBWA. |
Baada ya kukaa nje ya Ligi Kuu Bara kwa miezi
mitano, hatimaye beki wa kati, Juma Nyosso, amerejea kazini na kusaini mkataba
wa mwaka mmoja wa kuitumikia Mbeya City ya jijini Mbeya.
Nyosso baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia
Coastal Union ya Tanga msimu uliopita, hakuwa na timu, alikuwa akihusishwa
kurejea Simba lakini imekuwa tofauti.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji
huyo zinasema alishasaini na tayari yupo Mbeya kwa ajili ya kazi.
Kuhusiana na hilo, Nyosso na alisema: “Ndiyo
nipo Mbeya, nimeshasaini mwaka mmoja na hapa nipo kwenye mazoezi binafsi ila
tutaongea vizuri baadaye.”
SOURCE: CHAMPIONI







0 COMMENTS:
Post a Comment