March 5, 2015



Juhudi za kutaka kiungo Andrey Coutinho acheze mechi dhidi ya Simba zimeshindikana.


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema alimuachia daktari afanye kazi yake ili kuangalia kama Coutinho atacheza mechi ya Jumapili.

“Kwa hali ilivyo, inaonekana imeshindikana. Hivyo ataendelea na matibabu pia mazoezi lahisi.
“Baada ya mechi yetu na Simba, Jumapili tutaona hali yake inaendeleaje,” alisema Pluijm.

“Zile mechi za Mbeya zilikuwa ngumu sana, mchezaji yoyote angeweza kuumia, hivyo si jambo geni na tuna wachezaji wengine watachukua nafasi yake kama ilivyokuwa kule Botswana.”


Yanga ilisafiri kwenda Botswana kuivaa BDF katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho bila ya Mbrazili huyo. Ilipoteza kwa mabao 2-1, lakini ikasonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya ushindi wake wa 2-0 katika mechi ya kwanza jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic