April 27, 2015


Mkuu wa kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro alikuwa kama mtu aliyepagawa baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.

Yanga imetwaa ubingwa huo baada ya kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Muro alikuwa akiwangoza mashabiki wa Yanga huku akiwasha baadhi mwanga maalum ambao hutumiwa na mashabiki kushangilia.
Mashabiki wengine walikuwa wakishangilia pamoja naye huku wengine wakimpiga picha.

Mara kadhaa, Muro amekuwa akitamba kwamba Yanga ni ya kimataifa na leo alionekana kuwa na furaha zaidi kuthibitisha kauli yake hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic