Mwanasiasa maarufu wa Kenya, Raila Odinga leo
anatarajiwa kushuhudia mechi ya ufunguzi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame itakayozikutanisha Yanga na Gor Mahia ya Kenya kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Odinga ambaye ni kiongozi wa Chama cha Orange
Democratic Movement (ODM)’ ni shabiki mkubwa wa Gor Mahia atakuwa sambamba na
baadhi ya mashabiki wa timu hiyo waliosafiri kutoka Kenya kuja kuishangilia.
![]() |
| ODINGA... |
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Odinga
ambaye anayedaiwa kuwa na urafiki na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, atatazama
mechi hiyo kisha atakutana na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa
Tanzania.
Urafiki wa Magufuli na Odinga umethibitishwa
zaidi hivi karibuni ambapo waziri huyo aliyechaguliwa kuwania urasi wa Tanzania
kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenda Kenya katika mazishi ya mtoto
wa Odinga pia aliwahi kumuunga mkono katika kampeni za urais.
Pamoja na urafiki wake na Magufuli, Odinga ni rafiki wa karibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye imeelezwa huenda akaungana nao uwanjani katika mechi hiyo.
Manji aliwahi kumualika Odinga wakati wa ufunguzi wa maduka yake makubwa ya kibishara ya Quality Centre jijini Dar es Salaam.
Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
mchezo huo bila shaka ataiunga mkono Yanga ambayo ni Tanzania.









0 COMMENTS:
Post a Comment