September 5, 2015



MPIRA UMEKWISHAAAA
Dakika 4 za nyongeza
Dk 87, Bocco anarudi baada ya kutibiwa kwa dakika mbili baada ya kupasuka usoni

DK 84, Msuva anaingia vizuri katika eneo la hatari na kupiga shuti kali lakini linapita juu

Dk 82, krosi safi kabisa Bocco anapiga kichwa lakini mabeki Nigeria wanaokoa

SUB Dk Anatoka Farid nafasi yake inachukuliwa na Msuva
79 Dk 72 Bocco anapata nafasi nzuri na kupiga shuti kali lakini linaishia mikononi mwa kipa

SUB: DK 68, Stars wanafanya mabadiliko ya pili, anatoka Ngassa anaingia John Bocco

Dk 66, Nigeria wanapata kona baada ya kufanya shambulizi kali na Musa anapiga linaokolewa.
Dk 66, Ulimwengu akiwa amebaki kipa lakini anashindwa kufunga, shuti lake linaokolewa.
Dk 65 kwa mara nyingine tena, Stars wanapoteza nafasi nzuri kabisa. Ngassa akiwa na kipa anapaisha.

SUB Dk 60 Anatoka Mudathir anaingia Said Ndemla

Dk 59 Ulimwengu anabaki peke yake akiwa na kipa lakini anashindwa kuchangamka na kipa anawahi kuokoa na kuwa kona isiyozaa matnda.

Dk 56, Musa anapita tena na kwenda kasi lakini anashindwa kupiga vizuri
Dk 47, Musa anaingia ndani ya eneo la hatari na kupiga krosi nzuri lakini inaokolewa.

Dk 46 Nigeria wanafanya shambulizi kali, Barthez anaokoa na kuwa kona
MAPUMZIKO:

Dk 43&44 Stars wanapigiana pasi na kuwashinda Nigeria ambao ambao wanaonekana wazito.

Dk 42 Stars wanafanya shambulizi jingine, Nigeria wanaokoa tena
Dk 38, Barthez anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira uliopigw avizuri na kuwa kona. Lakini haijazaa matunda.


Dk 34, Nigeria wanafanya shambulizi kali lakini Barthez anafanya kazi ya ziadaDk 28, Ngassa anaangushwa eneo la hatari, lakini mwamuzi huyu kutoka Rwanda anasema hakuna kitu
Dk 22, Nigeria wanapiga faulo vizuri kabisa, Barthez naye anaokoa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Dk 18, Stars wanapata faulo baada ya Ngassa kaungishwa. Samatta anapiga faulo safi kipa anapangua huku wengi wakiamini lilikuwa bao.
Dk 14, Samatta anawatoka mabeki wawili na kupiga shuti kali, kipa anaokoa unamkuta Ulimwengu anapita unatoka nje goal kick

Dk 11, Musa anapiga krosi safi lakini Cannavaro anaokoa kwa kupiga kwa nguvu unatoka.
Dk 4, Stars wanapata kona, inachongwa vizuri lakini Nigeria wanaokoa.

Dk 3, Stars wanafanya shambulizi, Ngassa anaangushwa wanapata faulo.
Dk 1&2 Nigeria wanaonekana kuchangamka na 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic