October 29, 2020

 


NYOTA wa Simba, Bernard Morrison huenda ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaoihusu timu yake ya zamani ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7, Uwanja wa Uhuru.

 

Morrison mwenye pasi moja ya bao kati ya 14 yaliyofungwa na Simba kwa msimu wa 2020/21, alionekana akimpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Uhuru wakati timu yake ikichapwa bao 1-0.

 

Tukio hilo lilitokea baada ya mpira kusimama dakika ya 72, kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kuwa kwenye mzozo uliotokana na mwamuzi kuamua Simba ipige penalti baada ya mchezaji Luis Miquissone kuonekana akichezewa faulo ndani ya 18.


Kwa mujibu wa Kanuni ya 39,(21) kanuni za Ligi Kuu, Toleo la 2020, kuhusu udhibiti wa wachezaji inasema kuwa mchezaji yeyote atakayethibitika na kupatikana na hatia ya kumpiga mchezaji mwenzake isivyokuwa kawaida au kwa kutumia nguvu kubwa kuliko kawaida/kupigana ama kumpiga mwamuzi, kijana wa mpira, au ofisa, mhudumu mwingine wa mchezo atasimama kushiriki michezo isiyopungua mitano (5).

 

Kanuni hiyo inaeleza kuwa anaweza kufungiwa kati ya miezi mitatu mpaka mwaka mmoja na faini isiyopungua 1mil bila kujali hatua iliyochukuliwa na mwamuzi uwanjani na kwa mazingatio ya kanuni ya 39:5.3.

 

Hivyo ikiwa Kamati ya Maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania itatoa hukumu yake hivi karibuni ni wazi kuwa katika michezo mitano ambayo Morrison ataikosa ni pamoja na ule dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7.

 

Kama adhabu hiyo itatolewa kabla ya Simba hawajacheza mchezo wowote kuanzia sasa inamaana kuwa atakosa mchezo dhidi ya Mwadui, Kagera Sugar, Yanga, Dodoma Jiji na Polisi Tanzania.

 

Hata hivyo, anaweza kufungiwa zaidi ya hiyo au michache.Pamoja na kwamba mwamuzi hakuliona tukio hilo, lakini ni dhahiri kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia wa sasa, kamati hiyo inaruhusiwa kuangalia marudio ya mchezo huo na kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.

13 COMMENTS:

  1. Acha upuuzi wako unataka kuifundisha kamati ya maadili nn cha kufanya au kuilazimisha kukaa mapema Na kufuata ushauri wako,fanya kazi yako acha kutoa maoni yako Na kuyafanya kweli,shabiki zuzu WA yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bro kuna mda ukubali ukwel ww ni shabiki wa mpira na sio timu mashabiki kuna mda tujue kuwa kuna sheria za mpira

      Delete
  2. Huyu beberu anajifanya yeye ndo mwendesha mashitaka,yeye ndo shahidi,yeye ndo wakili,yeye ndo hakimu na tayari ameshahukumu kesi.

    ReplyDelete
  3. Mnaeleza ukweli mnaanza kumtukana mwandishi kosa lake nn mwandishi Jembe tupe vitu achana nao mashabiki maandaz . ...mtu umeona kabisa morrison kageuka mwakinyo alaf unaanza tukana

    ReplyDelete
  4. Mbona Morrison alipopigwa ngumi na mchezaji wa prison haukuandika haya?

    ReplyDelete
  5. Acha hayo wamesahau ya moro au wanataka watu waanze kufuatilia

    ReplyDelete
  6. Morriso kasajiliwa kuja kuigawa simbaikiwezekana mwisho wa dirisha la usajli atolewe kwa mkopo atuachie amani yetu,huyu jamaa hajaacha upuuzi kafanya hivyo alipokuwa yanga Leo anafanya Simba pia,kujinusuru nae nikumuondoa

    ReplyDelete
  7. Mikia fc yanapayuka tu hasa pale ukweli unapoelezwa , sasa hapo mwandishi kakosea nn

    ReplyDelete
  8. Huyu mwandishi ni mwanachama mwenye kadi ya utopolo story zake ni za kuuma na kupoza ila wakati mwingine mahaba yanazidi anajisahau

    ReplyDelete
  9. Subir uone Kama yatatokea hayo,,na Morrison lazma acheze mechi ya Simba vs yanga

    ReplyDelete
  10. Simba tulieniiii hivyo hivyo dawa iwaingieee morison on the beats

    ReplyDelete
  11. Dhambi ya dhuruma inawatafuna eti mchezaji ana mkataba mnapndisha sheria ili mumsaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic