Pamoja na klabu ya Simba kusisitiza mshambuliaji wake mpya, Laudit Mavugo ni mali yake, Vital’O ya Burundi, imeendelea kusisitiza inammiliki.
Vital’O imetuma nina lake kwenye Shirikisho la Soka la Burundi (BF) ikiwa ni sehemu ya wachezaji itakaowatumia msimu uliopita.
Hali hiyo inaashiria mgogoro wa usajili kwa Mavugo ambaye amejiunga na Simba msimu huu akielezwa kumaliza mkataba na timu yake hiyo ya zamani.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema, Mavugo hana tatizo lolote la usajili: “Ni mchezaji wa Simba na hakuna maelezo mengine zaidi.”
MAVUGO |
Lakini Rais wa Vital’O, Benjamin Bikorimana amesema, Mavugo hajamaliza mkataba na timu yake kama inavyoelezwa.
“Ni kitu cha kushangaza sana, Simba wanapoteza muda. ITC yake ipo kwetu, huyu ni mchezaji wetu na tuna mkataba naye, wanajisumbua,” alisema Bikorimana.
Kila mjanja ana mjanja mwenzie,sasa tuone hao mashoga kama watampata huyo Mavugo bila kutoa fedha!
ReplyDelete