December 10, 2016



DARASSA AKIWA AMESHIKA KOPI YA GAZETI LA MICHEZO, GAZETI LINALOMVUTIA ZAIDI KWA UPANDE WA MICHEZO NA BURUDANI NCHINI. ALIYENAYE NI
SALEH ALLY MAARUFU KAMA JEMBE.

Mashabiki wanaopenda Simba na Yanga yaani hawana upande mmoja mitaani huitwa tetesaklini wakifananishwa na dawa ya Tetracycline iliyokuwa na rangi mbili za njano na nyekundu.

Msaani Shariff Thabeet maarufu kwa jina Darassa anayetamba na ngoma yake ya Muziki, yeye anapenda zote Simba na Yanga lakini anavutiwa na uchezaji wa winga wa Yanga, Simon Msuva.

Darassa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na Global TV Online katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika Studio za TV hiyo zilizopo Bamaga jijini Dar es Salaam.

Alisema mbali na kuvutiwa na uwezo wa kutandaza soka wa Msuva pia amewahi kucheza naye wakati walipokuwa wadogo katika Uwanja wa Kijitonyama Muslim jijini Dar es Salaam.

“Mbali na muziki pia napenda sana soka kwani kati ya michezo ambayo huwa inaniburudisha lakini pia jambo la kushangaza mimi nazipenda timu zote mbili za Simba na Yanga na huwa napata shida sana pindi zinapokutana uwanjani.

“Lakini katika timu hizo kuna wachezaji ambao huwa napenda jinsi wanavyocheza na mmoja wao ni Simon Msuva, huyu nimecheza naye tulipokuwa wadogo hakika yupo vizuri,” alisema Darassa na kuongeza kuwa:


“Mbali na Msuva pia nimecheza na Said Ndemla wa Simba kwa sasa pamoja Abdallah Seseme (yupo Mwadui FC) ambao pia nilikuwa nikisumbuana nao tulipokuwa tukikutana uwanjani,” alisema Darassa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic