Na Saleh Ally
Makampuni mbalimbali yanayofanya kazi ya mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo yanamfanya kuwa mwanamichezo anayeingiza fedha nyingi zaidi kwa mwaka.
Ukiangalia katika maisha ya Ronaldo na fedha anazoingiza, unaweza kuona mwanamichezo mmoja anaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato kuliko watu milioni moja.
Kwa Tanzania inawezekana ikawa vigumu, lakini kama wachezaji watazidi kupata mafanikio zaidi kuna nafasi ya kubadilisha mambo na wao kujipatia fedha nyingi kupitia makampuni mbalimbali.
Lakini kufikia hilo, kunatakiwa mambo mengi muhimu. Kwani pamoja na kujituma, lakini nidhamu ya hali ya juu uwanjani na nje ya uwanja, vitu ambavyo wachezaji wengi wa Kitanzania wamekwama kabisa.
Ronaldo ni binadamu kama wengine, anaweza kufanya hivi, wako wanaofanya nusu yake, wengine robo yake na wanafanikiwa. Wachezaji wa Tanzania pia wanaweza kufanya angalau kiduchu sana na wakaondokana na maisha ya kulia na posho au mishahara iliyocheleweshwa.
Makampuni ambayo Ronaldo ameingia nayo mkataba wa kufanya nayo kazi hasa kujitangaza kupitia yeye ni Nike, Tag-Heuer, Sacoor Brothers, Monster headphones, MTG, Samsung, KFC, Emirates, Castrol, Herbalife, Poker Stars, ZTE, XTrade.com, Toyota, Armani, Unilever, Banco Espirito Santo, Mobily na Jacob & Co.
Lakini Ronaldo anaendelea kuingiza mamilioni mengine kupitia hotel anayomiliki pia kampuni yake ya mavazi ya CR7.
Mkataba wa Real Madrid: Novemba, Alisaini mkataba mpya na Real Madrid wenye thamani ya malipo ya mshahara kwa pauni 365,000 kwa wiki.
Nike: Amekuwa akidhamimiwa na kampuni kubwa ya vifaa vya michezo ya Nike tokea mwaka 2003. Ambayo inaelezwa aliingia nayo mkataba wa maisha yake yote unaokadiriwa kufikia pauni bilioni 1. Mwingine mwenye mkataba kama huo na Nike ni nyota wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA, LeBron James.
Armani: Kampuni hii ya mavazi ilimpa mkataba akichukua nafasi ya nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham ambaye alirithi jezi yake mamba 7 baada ya kutua Man United. Ronaldo amekuwa mwanaminitindo wa Emporio Armani hasa katika mavazi kama suruali.
Tag Heuer: Hii inajulikana bidhaa inayojumuisha watu wenye nazo yeye akiwa balozi, aliingia nayo mkataba 2014. Ndani yake inajumuisha mkataba wa Coca Cola na kwa mwaka anaingiza pauni milioni 22.
CR7: Hii ni kampuni yake binafsi ambayo inahusika na mavazi na zaidi imekuwa ikipewa nguvu na Nike na wakati mwingine kulipwa mamilioni ya fedha.
CR7 hotels: Ronaldo alitupia pauni milioni 54 katika uwekezaji katika hotel baada ya kuingia ubia na kampuni za Pestana Hotel Group.
Bei ya chumba katika hotel yake moja baada ya kuwa amezindua nne pauni 176 kwa siku. Hoteli yake ya jijini Lisbon, ina vyumba 82 vya bei hiyo wakati ina zaidi ya 10 vile via kifahari na kimoja tu katika hotel hiyo ya CR7 kinagharimu hadj pauni 882.
0 COMMENTS:
Post a Comment