Mwanariadha maarufu wa
Jamaica, Usain Bolt anatarajia kuweka rekodi mpya ya malipo pale atakaposhiriki
mashindano ya Diamond League yatakayofanyika katika kipindi cha joto jijini
Paris, Ufaransa.
Waandaaji wametangaza kuwa
Bolt atalipwa dola 10,000 (Sh milioni 16) kwa kila sekunde wakati akikimbia
mbio za Mita 200, Julai 6, mwaka huu.
Maana yake, Bolti
anatarajia kuingiza hadi dola 200,000 (zaidi ya Sh milioni 160) katika
mashindano hayo aliyokuwa hajashiriki tokea mwaka 2009.
Bolt alikuwa ameamua
kujitoa kushiriki mashindano karibu yote ya Ulaya kutokana na kukatwa kodi
kubwa kila anapokuwa anapokea malipo. Safari hii, waandaaji walifanya
mazungumzo na serikali ya Ufaransa na kufikia makubaliano ya kuondoa kodi hiyo.
Kwa malipo hayo, yanamfanya
kuwa mwanarisha anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko mwingine yoyote pia
mwanamichezo kwa ujumla anayelipwa kitita kikubwa zaidi katika kipindi kifupi
cha ushiriki wake wa michezo.
Mwanariadha huyo mwenye
kasi kuliko mwingine yoyote duniani pia anatarajkia kushiriki katika mbio za London
Grand Prix zitakazofanyika Julai 27 hasa kama suala la kodi litafanyiwa
marekebisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment