Pamoja na kuonekana haina nafasi ya kutosha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
England, Chelsea imeendeleza mbio za kutaka kutwaa kikombe cha FA baada ya
kuichapa Middlesbrough maarufu kama Boro kwa mabao 2-0.
Chelsea waliokuwa wageni katika Uwanja wa Riverside, walikwenda
mapumziko wakiwa hawana bao kama ilivyokuwa kwa wenyeji wao.
Kwa ushindi huo, Chelsea imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na
sasa itakutana na Man United.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Chelsea wakipeleka
mashambulizi mfululizo hadi walipopata bao katika dakika ya 51 kupitia Ramires
aliyepokea pasi ya Hazard ambaye kabla aliwahadaa walinzi. Shuti lake lilimgonga mgongoni Torres na kumpoteza kipa wa Boro.
Wenyeji walionekana kuchanganyikiwa, hata hivyo baadaye walichangamka
na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo na kuifanya Chelsea kuwa katika
wakati mgumu.
Wakati ikionekana kama Middlesbrough walikuwa wanakaribia kusawazisha,
Chelsea walipata bao la pili katika dakika ya 73 kupitia kwa Moses.
Bila ya ubishi, pamoja na kujaribu lakini ilionekana wenyeji hawakuwa
na njia tena ya kuing’oa Chelsea isisonge mbele katika michuano hiyo ya Kombe
la FA ambayo ina heshima kubwa nchini England.
VIKOSI:
Middlesbrough: Steele, Bailey, McManus, Bikey (Hines
35), Friend, Carayol (Zemmama 74), Leadbitter, Rhys Williams, Haroun, Main
(Miller 62), McDonald.Subs: Leutwiler, Emnes, Ledesma, Smallwood.
Chelsea: Cech, Ferreira, Ivanovic, Terry, Bertrand, Ake, Ramires, Moses (Luiz 76), Oscar (Marin 79), Benayoun (Hazard 58), Torres.
Subs: Turnbull, Cole, Lampard, Ba.
Mabao: Ramires 51, Moses 73.
ROBO FAINALI
Everton v Wigan
Manchester City v Barnsley
Millwall v Blackburn Rovers
Manchester United v Chelsea
0 COMMENTS:
Post a Comment