February 25, 2013




Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amesema fedha dola 35,000 (zaidi ya Sh milioni 55) alizolipwa na Malkia wa nyuki zimeingia katika akaunti yake nchini Serbia.

Milovan raia wa Serbia amesema fedha hizo tayari zimeingia ikiwa na maana tayari amepata malipo yake na ameshamalizana na Simba.

“Kila kitu kipo safi, nimewasiliana na mke wangu na kanihakikishia kwamba fedha zimeingia katika akaunti yangu. Kwanza nianze kumshukuru Malkia wa nyuki.

“Kutokea kwa huyo mama (Malkia wa Nyuki) imekuwa ni ahueni kwangu, nimeshukuru sana nimemalizana na Simba vizuri na ndicho nilitaka kwa kuwa nina marafiki wengi hapa, sikutaka hadi tufikie kushitakiana.

“Lakini nilikuwa sina ujanja, ilikuwa lazima nifanye hivyo. Lakini mama ameokoa mambo, nafurahi pia nawashukuru Wanasimba wote kwa kuniunga mkono tokea nikiwa kocha hadi nilipokuja kudai fedha zangu,” alisema.

Milovan anatarajia kuondoka nchini ndani ya siku mbili tokea leo kurejea kwao Serbia ambako atasubiri maombi ya kuzifundisha timu ambazo zitakuwa zimevutiwa naye.

Malkia wa Nyuki alijitokeza kumlipa Milovan baada ya uongozi wa Simba kuonekana ukisuasua kufanya hivyo licha ya kumpa ahadi kibao za kumaliza suala hilo, bila ya mafanikio.

Milovan alikuwa anadai dola 32,000 lakini Malkia wa nyuki alimlipa zaidi dola 3,000.

1 COMMENTS:

  1. simba mnatuabisha bhana malkia badala ya kufanya vitu vingine vya ndani ya klabu yeye analipa madeni jamani hebu kuweni na akili siku nyingine mtakosa wakujitolea kwaasababu ya uzembe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic