February 25, 2013




Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema presha yake kubwa imehamia katika mechi ya Jumamosi pale vijana wake watakapoivaa Kagera Sugar.
Manji amesema presha imekuwa juu kwa zaidi ya siku tatu kabla ya kuivaa Azam FC kwa kuwa ulikuwa ni mchezo muhimu sana na walitaka ushindi.

“Nafurahi vijana wamefanya vizuri na kushinda bao moja, kikubwa kwetu kilikuwa ni pointi tatu kwa kuwa ulikuwa ni mchezo muhimu sana.

“Ajabu sasa naona presha imerudi palepale na imehamia kwa Kagera Sugar, nataka kushinda kila mechi lakini ligi ni ngumu na upinzani uko juu sana.

“Lakini ninaamini tunaweza kufanya vizuri kwa kuwa wachezaji wamekuwa wakionyesha juhudi na viongozi wanafanya jitihada katika kuhudumia timu,” alisema.

Yanga ina pointi 39 kileleni, iwapo itaishinda Kagera Sugar keshokutwa, itakuwa imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa ambao watetezi wake Simba wanaonekana kusuasua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic