February 18, 2013


Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic juzi alitembelea na kuangalia namna gazeti la michezo la Championi linavyoandaliwa.
Milovan ambaye yuko nchini kudai fedha zake kwa klabu ya Simba, alitembelea ofisi za Global Publishers eneo la Bamaga, Dar es Salaam kwa mwaliko wa mhariri kiongozi wa gazeti hilo, Saleh Ally.
Milovan alipata nafasi ya kuuliza maswali na kujifunza namna maandalizi ya gazeti hilo bora la michezo linavyoandaliwa.
Kocha huyo raia wa Serbia amekuwa mdau mkubwa wa gazeti hilo pamoja na kwamba kiswahili chake cha kuzungumza kimekuwa ni cha 'kuungaunga'.
Milovan, baba wa watoto watatu wa kike, Ana, Sarah na Marta ameahidi kuendelea kujifunza kiswahili ili siku moja afaidi maneno yanayoandikwa kwenye Championi badala ya kuomba msaada wa tafsiri kila linapokuwa mkononi mwake

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV