February 24, 2013




Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza shilingi 239,686,000.

Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.

Kiingilio cha Sh 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha Sh 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza Sh 9,700,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja Sh 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi Sh 17,937,435.49, Kamati ya Ligi Sh 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh 8,968,717.75 na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) Sh 6,975,669.36.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic