February 26, 2013





Mourinho ataka mwamuzi wa El Classico aachwe
Kocha Mkuu wa Real Madrid, Jose Mourinho ametaka mwamuzi atakayechezesha mechi ya leo usiku dhidi ya Barcelona aachwe kabisa.

Katika mechi hiyo maarufu kama El Classico, Mourinho amesema wamejifunza mengi kuhusiana na mwamuzi walipokutana na Barcelona na akaonya wapinzani wake hao waachane na kuzungumzia kuhusiana na mwamuzi.
Lakini akaonya kwamba amesikia Barcelona wakizungumzia kuhusiana na mwamuzi, kitu anachoamini ni vizuri kila timu ikajipanga kucheza soka leo.

“Sidhani kama ni sahihi, kuanza kuwaza namna ya kusababisha upande mmoja upate kadi, badala yake tucheze soka. Ingawa tuliitaka sana mechi na Barcelona, lakini tuna jukumu zito tena dhidi ya Man United. Tunajua ni kazi ngumu lakini tutapambana.

“Mwamuzi awe mwenye haki na aachwe afanye kazi yake, mimi najua itakuwa ni mechi ngumu na gumzo,” alisema Mourinho.
 
Messi: Kelele zao hazitanichanganya
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesema wale wanaomlaumu kamwe hawawezi kumchanganya kabla ya kuwavaa Madrid leo.
“Najua kuna mechi ngumu mbele yetu, tunacheza na Real Madrid, timu yenye wachezaji bora na iliyokamilika kifiziki.

“Kupambana nao inataka ufundi, moyo wa kujituma na kupania kushinda. Lakini wanaolaumu hasa katika kipindi hiki, nafikiri wanataka kunichanganya. Watakuwa wanajidanganya, mimi na wenzangu tumeelekeza nguvu katika mechi hiyo,” alisema Messi.
“Mechi kama mbili hatukuwa katika kiwango kizuri, hatuna ujanja lazima turudi katika mechi dhidi ya Madrid, pia ni vizuri tushinde.”

Wachezaji Madrid kufika Barcelona siku ya mechi
Kikosi cha Real Madrid kitatua leo mjini Barcelona kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Mfalme, baada ya sare katika mechi ya kwanza mjini Madrid.

Uamuzi wa Madrid kutua leo na kuivaa Barcelona, kidogo umewashangaza wengi kwa kuwa hii ni mara ya kwanza mambo kwenda hivyo lakini Kocha Jose Mourinho anaamini ni uamuzi sahihi.

Wachezaji wa Madrid watapumzika hotelini kwa muda mchache kabla ya kwenda uwanjani kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.
Pamoja na hivyo, Mourinho amewashangaza wengi zaidi baada ya kufanya mazoezi na kikosi chake katika eneo la Valdebebas mjini Madrid na baada ya mazoezi akawaruhusu wachezaji kulala makwao.

Higuain kuanza, Kaka, Di Maria kugombea namba
Hadi jana usiku ilikuwa haijajulikana wachezaji 11 wa Real Madrid watakaoanza katika mechi ya leo ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona.

Jose Mourinho amesema hana uhakika ingawa dalili zinaonyesha ataanza na Higuain huku wawili, Ricardo Kaka aliyerejea uwanjani ana Angelo Di Maria wakigombea kuanza.
Mourinho ametamba kwamba katika kikosi chake kila mchezaji yuko fiti na anataka kucheza mechi hiyo, kitu ambacho ni bora kwake.

Mourinho amesema wachezaji watatangaziwa kikosi leo, ingawa amekwishawaeleza kila mmoja kujiandaa kwa kuwa yoyote anaweza kucheza tofauti na watu wanavyofikiria.


Fabregas: Hatuchongi sana kwenye vyombo vya habari
Kiungo wa Barcelona, Cecs Fabregas amesema wachezaji wa Barcelona hawana tabia ya kuzungumza sana na kulaumu kwenye vyombo vya habari.

Fabregas amewaambia waandishi wa habari kwamba wasingependa kuzungumza sana kuhusiana na mechi yao ya leo ya Kombe la Mfalme, badala yake watatoa majibu uwanjani.
Akizungumza kuhusiana na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu, Fabregas alisema wao wako katika hali nzuri na wanataka kucheza.

“Mfano mzuri unaweza kuwa Messi, unaona hazungumzi sana katika mikutano ya waandishi lakini majibu yake uwanjani.
“Anataka kucheza pia kushinda lakini kuinyoi mpira pia ni kitu muhimu. Hivyo subirini uwanjani tutafanya kazi yetu,” alisema Fabregas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic