February 25, 2013



Baada ya mashabiki wa Man United kuingia hofu kutokana na kuumia kwa mshambuliaji wao, Robin van Persie, sasa mambo yanaonekana kuwa ‘mswano’.
Van Persie alitolewa nje katika mechi ya Premiership wakati Man United ilipoivaa QPR baada ya kuumia karibu na kiuno baada ya kuanguka na kuigonga kamera, hali iliyozua hofu.

Lakini jana Jumatatu alionekana katika mitaa ya Alderley Edge akiwa na mpenzi wake, tena alionyesha kutokuwa na dalili yoyote ya maumivu.
Hali hiyo inaashiria Man United itakuwa na van Persie katika mechi yao muhimu ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mabingwa wa Hispania, Real Madrid siku chache zijazo.

Van Persie alipoulizwa kuhusiana na maumivu aliyokuwa nayo, alijivu kwa kifupi tu: “Nidyo, kila kitu kipo safi, namshukuru Mungu.”

Baada ya hapo, alitembea hatua chache na kuingia katika gari lake la kifahari aina ya Porsche na kuondoka zake.

Mholanzi huyo ndiye tegemeo la mashambulizi katika kikosi hicho cha Alex Ferguson na kawaida humpanga na Wayne Rooney, hali inayoifanya Man United kuwa tishio tokea kuanza kwa msimu huu.

 VAN PERSIE AKIONDOKA ZAKE...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic