Mmoja wa
viungo bora waliowahi kutokea nchini England, Paul Gascoigne amerejea nchini
humo na kusema Kocha Mkuu wa Manchester United, Alex Ferguson na mshambuliaji
wake, Wayne Rooney wamesaidia kuokoa maisha.
Mchezaji huyo
wa zamani wa Tottenham na timu ya taifa ya England, alikuwa Arizona nchini
Marekani kwa wiki tano akiwa anapata tiba maalum.
Gascoigne
maarufu kama Gazza alisema Ferguson alimtumia ujumbe na kumtaka aendelee
kupambana na maisha yake ya sasa kwa kuwa sima mazuri.
“Ferguson
aliniambia anatambua mimi ni mpambanaji, hivyo sipaswi kukata tamaa. Alisisitiza
niendelee kupambana na mambo yatakuwa mazuri,” alisema Gazza mwenye umri wa
miaka 45.
“Pamoja
na kuniambia maneno mengi ya upendo, Ferguson alisisitiza alikuwa akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wote wa Man United. Kweli imenifariji sana.
“Lakini
Rooney alijirekodi na kunitumia ujumbe wa picha, alinieleza anavyovutiwa na
mimi na anavyoamini nitarejea katika hali yangu nzuri.
“Alisema
siku akiwa na nafasi, atanialika ili niende kujumuika na wachezaji kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mechi.”
Gazza amekuwa akisumbuliwa na
ulevi wa kupindukia, hali inayomlazimu kupata tiba maalum ili kupunguza
unywaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment