Kiungo mzoefu wa vinara wa Ligi Kuu BaraYanga, Nurdin Bakari atafanyiwa upasuaji wa goti
wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya amethibitisha hilo leo, mara
tu baada ya mazoezi ya timu hiyo leo kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama.
Nurdin ambaye alijiunga na Yanga akitokea Simba misimu minne
iliyopita, amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti kwa muda mrefu sasa.
“Imekuwa ni muda sasa, lakini katika mazoezi ya jana
alijitonesha tena. Kocha akataka kujua, mwisho tukashauriana kuwa ni bora
kulimaliza kama hilo tatizo na matibabu sahihi ni upasuaji,” alisema Matuzya
aliyechukua nafasi ya Juma Sufiani.
Nurdin (kulia) mazoezini jana...
Vipimo vya goti la Nurdin kesho vitawasilishwa katika
hospitali ya Mwananyamala, baada ya hapo itapangwa hospitali ambayo atafanyiwa
upasuaji huo, wiki ijayo.
Katika siku za hivi karibuni, kiwango cha Nurdin kimeporomoka na imeelezwa majeruhi hayo yamekuwa yakichangia kwa kiasi
kikubwa.
Nurdin ni kati ya wachezaji wenye uwezo wa kucheza namba
nyingi uwanjani kama mbili, tatu, nne, tano, sita, saba tena kwa ufasaha.
0 COMMENTS:
Post a Comment