Waziri wa Afya, Dk Hussein Mwinyi leo asubuhi amemtembelea
kumjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda aliyelazwa
akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari ambao
pia wanachapisha magazeti ya michezo ya Dimba na Bingwa, usiku wa kuamkia leo alishambuliwa
na watu wasiojulikana.
Ingawa watu hao wanaaminika kuwa ni majambazi, lakini
imeelezwa hawakupora kitu chochote ndani ya gari lake, mfano simu na kompyuta
mpakato (laptop).
Kibanda aliumizwa na watu hao ambao walimvamia wakati
akiingia nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam. Wakavunja kioo cha gari na
kumtoa nje kabla ya kuanza kusmhambulia ikiwa ni pamoja na kumkata mapanga
kichwani na kulijeruhi vibaya jicho lake, pia imeelezwa wamemyofoa kucha.
Kibanda ameumizwa vibaya jichoni, tayari madaktari
wameonyesha hofu ya jicho hilo kurudi katika hali yake ya kawaida na uwezo wa
kuona tena. Hata hivyo wamekuwa wakiendelea na juhudi.
Kabla ya kurejea New Habari, Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji
wa Free Media wanaochapisha gazeti la Tanzania Daima na Sayari, kabla ya hapo
alikuwa Mwananchi Communications.
JEMBEBLOG INAKUPA POLE KIBANDA NA KUMUOMBA
MUNGU AKUSAIDIE UREJEE KATIKA AFYA NJEMA.
0 COMMENTS:
Post a Comment