*Wamfuata
airport, yeye agoma kujibu maswali yao
Waandishi
Waingereza waliamka alfajiri na mapema siku iliyofuata baada ya Man United
kutolewa na Real Madrid na kufunga safari hadi Uwanja wa Ndege wa Manchester
ili kuzungumza na mwamuzi Cuneyt Cakir.
Cakir
raia wa Uturuki, hakuwa tayari kuzungumza lolote pamoja na waandishi hao kuwa
wamemuandalia maswali. Akiongozana na wenzake wanne, aliwaacha solemba.
Hasira za
waandishi hao zikamalizikia kwenye uchunguzi na kugundua Cakir amekuwa mahiri
kwa kutoa kadi katika mechi za Ligi Kuu ya Uturuki na anasifika kwa kuboronga
mechi zake.
Pia
walionyesha ambavyo amekuwa mmoja wa marafiki wa Ronaldo wa real Madrid katika
mtandao wa kijamii wa Twitter, wakianisha kama moja ya vigezo vya Cakir
kuboronga mchezo huo wa hatua ya 16 Bora ambao ulimalizika kwa wageni Real
Madrid kushinda kwa mabao 2-1, la ushindi likiwa limetupiwa na Ronaldo.
Cakir
alimtwanga Nani wa Man United kadi nyekundu moja kwa moja baada ya kumkanyaga
Arbeloa wa Real Madrid, lakini mjadala umekuwa mkubwa wengine wakiamini mwamuzi
huyo hakuwa sahihi.
Mjadala ni
mkubwa kwa kuwa wako wengi wanaopinga, lakini wako wamekuwa wakisisitiza kwamba
Cakir alikuwa sahihi kumpa kadi hiyo Nani, kwani pamoja na kutomuona Arbeloa,
baadaye aliongeza kumkanyaga kwa makusudi.
Rekodi zilizopatikana
zimeonyesha Cakir hajawahi kuchezesha mechi yoyote bila ya kutoa kadi. Inaelezwa
tokea Januari, mwaka huu tayari alikuwa ametoa kadi 36 za njano, tatu nyekundu.
Hizo amemwaga katika mechi nane tu za ligi alizochezesha.
Mechi yake
ya mwisho ya ligi kwao Uturuki kabla hajafunga safari kwenda Uingereza
kuchezesha mechi hiyo katika Man United dhidi ya Real Madrid, Cakir alimwaga kadi sita za njano katika mechi hiyo
iliyowakutanisha Akhisar Beledi dhidi ya Elazigspor.
Waingereza
hao wamezidi kuangusha makombora kwamba Cakir hajawahi kupewa mechi kubwa msimu
huu, mara ya mwisho ilikuwa mechi ya Super Cup kati ya vigogo wa Uturuki, Galatasaray
dhidi ya Fenerbahce, Agosti, mwaka jana.
Uthibitisho yeye ni rafiki wa Ronaldo kwenye Twitter...
- Unafikiri ulifanya vizuri kazi yako siku ya mechi?
- Unajuta kutokana na kadi uliyompa Nani?
- Ferguson alikuambia kitu kipi wakati wa dakika zote za mchezo?
- Je, unatarajia kurejea Old Trafford?
- Je, unatarajia kupata kadi ya Krismas kutoka kwa Rio Ferdnand?
0 COMMENTS:
Post a Comment