Wakati inaendelea
kupambana kuokoa roho yake, ili ibaki katika Ligi Kuu England, klabu ya Reading
imetangaza kumtimua kazi kocha wake mkuu, Brian McDermott.
Readind
iliendelea kudidimia katika msimamo wa Premiership baada ya kufungwa mabao 2-1
na Aston Villa, Jumamosi iliyopita.
Imeelezwa,
McDermott amechanganikiwa na uamuzi huo wa klabu baada ya siku 33 zilizopita
kufanikiwa kutangazwa kocha bora wa Premiership.
Muitaliano
Paolo Di Canio anaelezwa ni kati ya wanaopewa nafasi ya kuwa makocha wa Reading
na Jumamosi alikuwa uwanjani wakati Reading ikipambana na Aston Villa.
Mmiliki
wa Reading, Anton Zingarevich alitoa shukurani kwa kocha huyo ambaye amekuwa na
mafanikio makubwa katika klabu hiyo tokea alipoanza kuifundisha mwaka 2009.
Brian aliisaidia
Reading kupanda daraja hadi Premiership ikiwa ni mara ya pili katika historia
ya klabu na inaonekana kutokana na mambo yanavyokwenda, klabu hiyo haiwezi
kukwepa kuteremka.
Premiership
ina timu 20 huku Reading ikiwa katika nafasi ya 19 na pointi 23 sawa na QPR
inayoburuza mkia.
McDermott
amewahi kuichezea Arsenal katika mwanzo mwa miaka ya 1970 akiwa mmoja wa viungo
mahiri, baadaye akajiunga na Fulham.
Msimu wa
2011-12 alionyesha ni mmoja wa makocha bora baada ya kuipa timu hiyo ubingwa wa
Ligi Daraja la Kwanza England maarufu kama Championship.
0 COMMENTS:
Post a Comment