Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope
ametangaza kujiuzulu katika nyadhifa hiyo.
Hans Pope aliyekuwa jembe la usajili la Simba, amesema
ameamua kuachia nafasi yake hiyo kutokana na mambo yanavyokwenda.
Mapema asubuhi leo Hans Pope alisema: “Subiri kidogo nitakupa
jibu.”
Alipopigiwa baada ya saa moja akasema: “Niko njiani nakwenda
ofisini, nikifika nitaandika barua ya kujiuzulu halafu nitaiwasilisha.”
Alipotafutwa saa nane mchana leo, akajibu: “Kweli,
nimeshaandika barua na kuiabidhi, tayari nimejiuzulu.”
Uongozi wa Simba kupitia Katibu Mkuu, Evodius Mtawala,
umethibitisha kujiuzulu kwa Hans Pope ambaye amesema mambo yamekuwa hayaendi
vizuri na kwa mpangilio.
Kujizulu kwake ni pigo kwa Simba ambayo imekuwa ikienda kwa
mwendo wa kuyumba huku ikiwa haina nafasi ya kutetea ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment