March 7, 2013



Ismail (mwenye fulana nyeupe), akituatilia mazoezi ya Yanga..

Mshambuliaji kinda wa Simba, Rashid Ismail ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akijitokeza katika mazoezi ya Yanga, alisema anavutiwa na mazoezi tu.


Akizungumza na Salehjembe, Ismail alisema anavutiwa na mazoezi ya Yanga ndiyo maana hupenda kwenda kuangalia ikizingatiwa anaishi karibu na Uwanja wa Bora ambao Simba wanafanyia mazoezi.

“Ninakuja mazoezini hapa kuangalia, hakuna kitu kingine. Wachezaji wengi wa Yanga ni rafiki zangu, sasa ubaya uko wapi,” alisema.
Mara ya kwanza alipotua uwanjani hapo, nusura baadhi ya mashabiki wa Yanga waliokuwa mazoezini hapo wamvamie wakiwa na hofu huenda angewahujumu.

 Akimsalimia beki wa Yanga, Juma Abdul...
 Akiwa jirani na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto...
Akiwa na Malkia wa Nyuki mjini Muscat..
Lakini juzi, Ismail aliibuka tena na kushuhudia mazoezi hadi mwisho, akasalimiana na wachezaji wa Yanga na kuondoka zake.

Inaelezwa Ismail amewahi kucheza Yanga B kabla ya kujiunga na kikosi cha watoto wa Simba ambao walipata sifa kubwa chini ya Selemani Matola kutokana na kutandaza soka la uhakika ikiwa ni pamoja na kutwaa Kombe la BancABC huku wakiwatoa shoo wakongwe kama Mtibwa Sugar na Azam FC.

Ismail alikuwa katika kikosi cha Simba kilichoweka kambi ya wiki mbili nchini Oman na katika mechi ya mwisho ambayo ni pekee waliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya al Sidab, Kocha Patrick Liewig alimuamini na kumuanzisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic