Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Simba, Rahma Al Kharusi
maarufu kama Malkia wa Nyuki amesema Simba inapaswa kujipanga kwa ajili ya
msimu ujao.
Malkia wa Nyuki amesema kimahesabu inaonekana Simba imepotea
lakini haitawakatisha tama kuhakikisha inafanya vizuri angalau mechi
zilizobaki.
“Lazima tuwe waungwana na kuangalia hali inavyokwenda, Simba haiku
vizuri na mambo mengi hayakwenda vizuri lakini hatuwezi kukata tamaa na kuacha
kila kitu kiende hovyo.
“Ninaamini tukishirikiana tunaweza kumaliza mambo angalau
vizuri na msimu ukaisha tukiwa na nafasi nzuri hata kama tutakuwa tumekosa
ubingwa. Lakini msimu unaokuja ndiyo tunatakiwa kuulenga.
“KIla kitu tunatakiwa kufanya mapema ili kujipanga vizuri,
utaona mambo kidogo si mazuri ndani ya klabu lakini Wanasimba wanapaswa kuwa na
subira na kujipanga ili mambo yarekebishwe,” alisema Malkia wa Nyuki.
Wiki iliyopita, Malkia wa Nyuki aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Ushindi ya Simba lakini siku chache baadaye, makamu wake, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ akajiuzuru nafasi ya umakamu mwenyekiti wa Simba.
Lakini kabla ya hapo, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo,
Zacharia Hans Pope ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili naye akabwaga
manyanga.
Mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage ambaye yuko katika matibabu nchini India naye anabwaga
manyanga.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wamekuwa wakisuasua katika nafasi ya tatu wakati Yanga na Azam FC ndiyo wanaoonekana wametulia zaidi katika mbio za kuwania ubingwa huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment