March 9, 2013




Ismail akiwa na Mrisho Ngassa...
Simba inaendelea kuongoza kwa skendo za kutolipa wachezaji wake baada ya kubainika mshambuliaji wake kinda, Rashid Ismail anadai mishahara ya miezi mitano.

Ismail ambaye hivi aliibuka katika mazoezi ya Yanga wakati akiwa mchezaji wa Simba, imeibainika anadai mshahara wa miezi mitano.

Rafiki wa karibu wa Ismail ameeleza kinda huyo anadai mishahara hiyo pamoja na wachezaji wengine makinda na uongozi umekuwa ukiwazungusha.

Juhudi za kuwapata viongozi wa Simba, jana jioni hazikufua dafu lakini Ismail mwenyewe alikiri kwamba anadai lakini akakataa kuzungumzia zaidi.

“Kudai nadai, lakini nisingependa kuzungumza kwenye vyombo vya habari,” alisema.
Hivi karibuni uongozi wa Simba uliwalipa wachezaji wake mshahara wa Januari wakiwa Arusha kujiandaa na mechi dhidi ya Libolo.

Lakini basi lao likazuiliwa na mwenye hoteli jijini Arusha ambaye alikuwa anadai Sh milioni 15 kabla ya Malkia wa Nyuki hajaokoa jahazi.

Lakini Malkia wa Nyuki aliwaokoa tena viongozi wa Simba kwenye aibu ya deni la aliyekuwa kocha wake, Milovan Cirkovic na kutoa zaidi ya Sh milioni 50 kumlipa Mserbia huyo aliyekuwa anadai mshahara wa miezi minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic