March 4, 2013




Msimbazi leo mchana..................PICHA NA SHEBY MKASSY

Baada ya Simba kuchapwa mabao 4-0 na Libolo jana mjini Calulo, Angola kuna taarifa mashabiki wa Simba wameanzisha mzozo kwenye makao makuu ya klabu hiyo.

Mashabiki na wanachama mchana huu wamejazana kwenye makao makuu ya klabu hiyo barabara ya Msimbazi na kuanza kupiga kelele wakitaka Mwenyekiti, Ismail Aden Rage aondoke.
Wanachama hao wa Simba wameonekana wakilalama na kudai uongozi wa Rage ndiyo umekuwa tatizo kubwa.



Pamoja na Rage wanachama hao wamesisitiza kwa mara nyingine makamu wake, Geofrey Nyange maarufu kama Kaburu naye aondoke.
Simba ilifungwa mabao manne jana na kutolewa kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya kuwa imefungwa kwa bao 1-0 nyumbani Dar katika mechi hiyo ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ilianza kuyumba katikati ya msimu hata kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara. Baadaye uongozi ukamtimua Kocha Milovan Cirkovic kwa madai kwamba amezembea.

Lakini tokea ameondoka na kutua kwa Mfaransa, Patrick Liewig, mambo yamezidi kuwa magumu kwa Simba ambayo imekuwa ikishinda mechi moja na kusubiri kipigo au sare.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic