March 4, 2013




Mabingwa wa Hispania, Real Madrid wametua jijini Manchester na mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo na Kocha, Jose Mourinho wamekuwa kivutio kikubwa.

Mashabiki wengiw aliojitokeza uwanja wa ndege walionyesha wazi walitaka kuwaona watuw awili tu, Ronaldo na Mourinho ambao walishangiliwa kwa nguvu wakati wakipita kuingia kwenye basi.



Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kurejea Man United ambayo ni klabu yake ya zamani alishangiliwa zaidi ikiwa ni dalili za kukaribishwa tena katika klabu hiyo. Mashabiki hao walionyesha kutojali kwamba Ronaldo atakuwa na kazi ya kupambana na klabu yao kesho usiku.

Madrid ambayo iko nchini humo kupambana na Man United katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora baada ya sare ya bao 1-1 jijini Madrid.
Tayari Madrid wameanza mazoezi na wamekuwa wakifanya katika uwanja wa Etihad unaomilikiwa na wapinzani wakubwa we Man United, Manchester City.

Imeelezwa Old Trafford hauko katika hali nzuri, hivyo ulikuwa ukifanyiwa matengenezo kabla ya mechi ya kesho ambayo inasubiriwa kwa hamu baada ya Madrid kuonyesha iko katika kiwango cha juu kwa kuwafunga wababe wa Man United, Barcelona mara mbili mfululizo ndani ya siku nane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic